Dk Samia: Uteuzi Mwigulu Nchemba ulikuwa na ushindani - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 14 November 2025

Dk Samia: Uteuzi Mwigulu Nchemba ulikuwa na ushindani

 


Waziri Mkuu Mwigulu lameck Nchemba akiapa




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amemuapisha Dkt Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu, akimweleza uteuzi wake umepitia ushindani mkubwa.




Hata hivyo, Dkt Samia amesema licha ya kuwa na ushindani mkubwa, lakini katika vigezo kadhaa, Dkt Mwigulu amewashinda wenzake kwa sifa kidogo kuliko wengine alioshindana nao.



Dkt Samia ameeleza hayo, leo Ijumaa Novemba 14, wakati akimuapisha Waziri Mkuu mpya, Dkt Mwigulu Nchemba aliyemteua jana na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Hafla ya kumuapisha Dkt Mwigulu imefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodomo na kuhudhuriwa na viongozi wakuu waandamizi wa Serikali na wastaafu.
“Vigezo vyote vilivyopimwa, tumepima katika maeneo mbalimbali vya kuitumikia nchi hii na kulitumikia Taifa hili. Kubwa zaidi ni kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”



No comments: