KISWAHILI LUGHA RASMI UNESCO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 11 November 2025

KISWAHILI LUGHA RASMI UNESCO




Balozi wa Tanzania 🇹🇿 nchini Ufaransa 🇫🇷 Mheshimiwa Ali Mwadini ameelezea furaha yake baada ya lugha ya Kiswahili kutangazwa kuwa lugha rasmi kwenye Mikutano yote ya UNESCO…

“Ninayo furaha ya kuwaletea habari njema ya kupitishwa kwa sauti moja, Azimio la Mkutano Mkuu wa UNESCO la kuitambua lugha ya Kiswahili kama moja ya lugha rasmi za Mkutano Mkuu wa UNESCO” amesema Balozi Mwadini…

Azimio hilo limepitishwa leo tarehe 11 Nov. 2025, Jijini Samarkand, Uzbekistan 🇺🇿, ambako Mkutano Mkuu wa UNESCO unaendelea, kufuatia pendekezo lililowasilishwa na Tanzania 🇹🇿, mapema mwaka huu…

Hongera sana Balozi wetu!… 🙏🏾


No comments: