Mbunge wa Monduli "Kadogoo"atinga bungeni na Ari mpya. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 11 November 2025

Mbunge wa Monduli "Kadogoo"atinga bungeni na Ari mpya.

Mbunge Mteule wa Monduli, Izack Joseph Copriano (Kadogoo) akiwasili Bungeni mapema leo

Mbunge Mteule wa Monduli, Izack Joseph Copriano (Kadogoo) sitibya nyumba akiwa ndani ya Bunge


Mwandishi wetu,Dodoma

maipacarusha@gmail.com


Mbunge Mteule wa Monduli, Izack Joseph Copriano (Kadogoo), ashiriki kikao cha kwanza cha Bunge la 13 jijini Dodoma huku akiwa na Ari mpya kuwatumikia wakazi wa Monduli.


Izack Joseph Copriano, maarufu kama Kadogoo, Mbunge mteule wa Jimbo la Monduli (CCM), leo tarehe 11 Novemba 2025, ameshiriki kwa mara ya kwanza kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma.


Kikao hiki ni sehemu ya Bunge la 13, ambacho kimeanza leo na kujumuisha wabunge wapya pamoja na wale waliorejea, wakitarajiwa kuapa katika siku chache zijazo kabla ya kuanza rasmi majukumu yao.


Kadogoo, ambaye kabla ya kugombea ubunge alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli alipata ushindi wake wa kishindo Oktoba 29, 2025, ameonekana akiwa na ari, nidhamu na hamasa kubwa ya kulitumikia Taifa, huku akisisitiza dhamira yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Monduli .


Katika kampeni zake miongoni mwa ahadi zake zilizompa ushindi ni kutatua kero ya maji na kumaliza migogoro ya ardhi Monduli huku akiahidi kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya lakini pia suala la elimu likiwa kipaumbele kikubwa.


Mwisho







No comments: