MBUNGE WA JIMBO LA BUTIAMA AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 11 December 2025

MBUNGE WA JIMBO LA BUTIAMA AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU

 




Na Onesmo Mbise, Butiama 


maipacarusha@gmail.com


Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Wilson Mahera, amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu katika Kata ya Kamugegi, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, ambapo mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya jimbo hilo.


Uzinduzi huo uliofanyika tarehe 10 Desemba 2025, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata akiwemo Diwani wa Kata ya Kamugegi, Mhe. Wilson Kinguye, pamoja na Diwani wa Kata ya Buruma, Mhe. Mogela Mbonosi.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Mahera alisema mashindano hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Butiama yamelenga kukuza vipaji vya vijana, kuimarisha upendo na kudumisha umoja katika jimbo zima.


 "Ofisi ya Mbunge ina dhamira ya kuijenga Wilaya ya Butiama kupitia michezo ili kukuza vipaji vya vijana na kujenga umoja na mshikamano kwa wananchi wa Jimbo la Butiama,"alisema Dkt. Mahera.




Mashindano hayo yataanza katika ngazi ya vijiji, kisha kata, na hatimaye ngazi ya wilaya, ambapo kata zote 18 za Jimbo la Butiama zitashiriki ili kumpata timu bora itakayowakilisha jimbo hilo.


Aidha, mashindano hayo yanayodhaminiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Butiama ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano, mshikamano, amani, umoja, afya na kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.

No comments: