Na Mwandishi Wetu.Maipac
maipacarusha20@gmail.com
UCHAGUZI wa katibu wa madiwani wa Chama cha mapinduzi(CCM) Manispaa ya Morogoro uliofanyika Desemba 16,2025 umelalamikiwa na baadhi ya madiwani kuwa haukuwa wa haki na haukufuata taratibu.
Taratibu hizo ni pamoja na kuletwa kwa jina moja la mgombea naye ni diwani wa vitu maalumu Salma mbandu ambaye inadaiwa alipigiwa kura nyingi za hapana lakini Cha kushangaza alitangazwa kuwa ameshinda kwa kupata kura nyingi za ndio.
Aidha inadaiwa katika nafasi hiyo ya katibu wa madiwani wa CCM diwani vitu maalumu Warda Bazia alichukua fomu kuomba nafasi hiyo lakini jina lake halikurudishwa.
Baadhi ya madiwani walieleza kutoridhishwa na mwenendo mzima wa kupatikana kwa nafasi ya katibu wa madiwani, ikiwemo ya kutakiwa kuchukua fomu kwa kiasi cha shilingi 100,000 jambo ambalo si utaratibu huku wajumbe wa kamati hiyo wakitakiwa kuchukua fomu kwa shilingi 50,000.
Diwani Bazia akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo alisema, ameshangazwa na kutorudi kwa jina lake kwani amekuwa diwani kwa awamu ya tatu sasa hajawai kuwa na utovu wa nidhamu ndani ya chama chake na hajawahi kufikishwa kwenye kamati ya maadili.
"Sijawahi kufika kamati ya maadili na kama walikuwa wanamtaka mtu wao kwa Nini waliweka kigezo Cha watu kuchukua fomu, na miaka yote madiwani tunachagua wenyewe katibu bila kuingiliwa na Wala hakuna suala la kulipishwa fedha safari hii sekretarieti ndo imeingilia kati na kufanya yasiyofaa,"alisema Warda Bazia.
Alisema uchaguzi huo miaka yote haunaga mchujo na kwamba gharama ya kuchukua fomu imewekwa kubwa na nafasi hiyo hainaga maslahi akashangazwa fedha hiyo kulinganishwa na fomu ya kipindi cha udiwani.
Baadhi ya madiwani hao walisema wakiwa kwenye kikao hicho Cha kumpata katibu huyo walihoji na kuletewa ubabe ambapo sekretarieti iliongozwa na katibu wa Vijana Halid King.
Warda alisema wao hatua waliyochukua ni kupeleka malalamiko yao kwa katibu wa CCM mkoa ambaye aliwaeleza kuwa anasubiri muhtasar¹1i wa CCM Wilaya ndo atashughulikia.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja hivi karibuni akizungumza kwa njia ya simu alisema wanaojitangaza kuwa tayari wamepitishwa kuwa katibu wa madiwani hawajiamini na hawafai kuwa viongozi.
"Hao Wanaojitangaza hawajiamini na hawafai kuwa viongozi ndio sababu wanadai kusimamiwa na viongozi wa juu ili wasipate ushindani,"alisema Ngereja.
Ngereja alisema katibu wa madiwani kawaida anateuliwa na madiwani wenyewe miongoni mwao na chama jukumu lake ni kutoa maelekezo jinsi ya kumpata katibu wao.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment