Nyuki kudhibiti Tembo Tarangire na kuongeza mapato kwa wananchi. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 17 December 2025

Nyuki kudhibiti Tembo Tarangire na kuongeza mapato kwa wananchi.

     




 


Mkurugenzi wa shirika la tembo pilipili, Dr Alex chang’a

Mizinga ya Nyuki inayotumika kama kizuizi cha tembo kuvamia mashamba ya wakulima

 

Mussa Juma,Tarangire.


maipacarusha@gmail.com


Wananchi wanaopakana na hifadhi ya Taifa ya Tarangire wilayani Babati mkoani Manyara ,wamepewa mafunzo ya kuzuia Tembo wasivamie na kuharibu mazao, kwa kutumia nyuki lakini pia watapata kipato kwa kuuza asali na mazao mengine ya Nyuki.


Mafunzo hayo yametolewa na Shirika lisilo la kiserikali la TEMBO PILIPILI kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) katika kijiji cha Kakoi wilayani Babati yakilenga pia kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori na kuboresha maisha ya wananchi.




Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa shirika la tembo pilipili, Dr Alex chang’a, amesema elimu hiyo itawawezesha wananchi kulinda mazao yao huku wakitumia uhifadhi na utalii wa kitamaduni kama fursa mbadala ya kipato.


C9

ZzZMeneja wa mpango wa maendeleo ya maisha wa shirika hilo Jeremiah Julias amesema wananchi watanufaika na utalii wa kitamaduni kwa kupata fursa ya kuuza bidhaa za asili ikiwemo asali, kuvutia watalii kutembelea maeneo yao, na hivyo kuongeza kipato na kukuza uchumi wao.


"Huu mradi tunatarajia utakuwa na matokeo mazuri wananchi wapata mavuno ya mazao lakini pia watauza usali na mazao mengine ya nyuki"alisema.

Meneja wa mradi huo, Francis Ndemela

Meneja wa mradi huo, Francis Ndemela alisema tayari mizinga imefungwa kuzunguka mashamba na baadhi tayari ina nyuki.


"Manufaa ya mradi huu utasaidia kuendeleza pia uhifadhi na utalii na wanufaika wakubwa ni kina mama"alisema


Afisa Wanyamapori wilaya ya Babati, Emmanuel laizer aliwataka wakazi wa kijiji hicho kutunza mradi huo kwani unamanufaa makubwa.


Laizer alisema mradi huo ndio suluhu ya kupunguza migogoro ya Tembo kuvamia mashamba na makazi yao.

Wanufaika wa mradi

Baadhi ya wananchi walioshiriki mafunzo hayo walisema Elimu Hiyo itawasaidia kulinda mazao, kuongeza kipato na kujiajiri, hasa kwa vijana na wanawake.


Lemanya Mollel alipongeza Tembo pilipili na serikali kwa kupeleka mradi huo katika kijiji chao.








Mwisho



No comments: