ADAIWA KUJIUA KWA KUJIKATA KOROMEO AKIWA NYUMBA YA KULALA WAGENI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 27 January 2026

ADAIWA KUJIUA KWA KUJIKATA KOROMEO AKIWA NYUMBA YA KULALA WAGENI

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama 

Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


GIDION Mbwambo(34)mkazi wa Manispaa ya Morogoro amekutwa amejiua kwa kujikata Koromeo kwa kutumia kitu chenye makali kwenye nyumba ya kulala wageni na inadaiwa alikuwa amelewa.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema hayo wakati alitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mjini Morogoro.


Mkama alisema tukio hilo lilitokea Januari 27,2026 Majira ya asubuhi katika nyumba ya kulala wageni ya Kisanga iliyopo mtaa wa nguzo Kata ya Mazimbu.


Alisema marehemu alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba namba 106 Januari 26,2026.


Kamanda Mkama alisema iligundulika baada ya michilizi ya damu na maji ikitokeza nje ya chumba alichopanga marehemu.


"Baada ya kuvunjwa mlango uliokuwa umefungwa kwa ajili ya uchunguzi ilibainika alikufa na alikuwa na jereha la kujitaka Koromeo eneo la shingo kwa kutumia kitu chenye makali,"alisema.


Kamanda alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu amejiua kwa kutumia kifaa hicho na kwamba alikuwa katika hali ya ulevi.


Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limetoa wito kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwa makini na kufuata taratibu zote za kutambua wageni,ili inapotokea changamoto kama hiyo iwe laisi kutambuliwa.


Mwisho.

No comments: