![]() |
Na mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema amechagua kupanda miti katika siku yake ya kuzaliwa ili kutimiza wajibu wake wa kuitunza na kuhifadhi sayari ya dunia.
Sambamba na hilo, Dk Samia ameeleza kuwa ameamua kusheherekea ‘birthday’ yake kwa kupanda miti ili kuacha urithi kwa vizazi vinavyokuja.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 27, 2026 wakati akisheherekea siku ya kuzaliwa kwake iliyoambatana na upandaji miti, sambamba na kukata keki, hafla iliyofanyika Bungi Kilimo Kizimkazi, Zanzibar.
“Sisi turirithi uoto wa asili mwingi sana, tulirithi nchi yetu ambayo haikuwa imeharibiwa kiasi hiki. Turirithi miti mingi ya matunda iliyopandwa shambana na mingine kujiotea,” amesema na kuongeza kuwa:
“Lakini leo mtoto wetu akitaka kula pera lazima akalinunue sokoni. Sisi tulikuwa tunapita msituni na kula mapera ya aina yoyote tunayotaka,” amesema Dkt Samia.
Kwa mujibu wa Dkt Samia, hivi sasa miti hiyo imepotea hivyo ni wajibu kwa kila Mtanzania kurudisha uoto wa asili na miti ya asili ili kuleta urithi kwa watoto.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa nchi, amemeshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kumpa afya ya njema na kuiona kwa mara nyingine Januari 27, akiwatakia kheri Watanzania wengine waliozaliwa tarehe kama hiyo.


No comments:
Post a Comment