CAMFED YAWANUFAISHA WASICHANA 83,000 WANAOTOKA FAMILIA DUNI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 29 January 2026

CAMFED YAWANUFAISHA WASICHANA 83,000 WANAOTOKA FAMILIA DUNI





Na Lilian Kasenene Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


WASICHANA 83,000 kutoka kwenye mazingira magumu katika  mikoa 10 ya Tanzania wamenufaika na kupata misaada mbalimbali ya ujasiliamali kupitia shirika la CAMFERD Tanzania linalojihusisha kusaidia watoto wa kike wanaotoka kwenye mazingira hayo na familia duni.


Akizungumzia mafanikio ya wasichana hao kwenye mahojiano baada ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka 2025 uliofanyika mkoani Morogoro mkurugenzi Mtendaji wa CAMFED Tanzania Anna Sawaki alisema mafanikio hayo ni makubwa kwa Shirika na wanaendelea kutoa msaada.


Sawaki alisema camferd kwa kushirikiana na serikali wamejipanga kuhakikisha vijana wanapata baadhi ya wadau wa kuwasaidia vitendea kazi mbalimbali ili waweze kukuza biashara zao.


Alisema wasichana hao bado wanauhitaji wa kusaidia katika kukuza mifumo ya biashara, masoko na kuongezewa thamani kwa wale wanaofanya biashara ya kilimo hasa wanaolima kilimo cha kisasa ambao wameibuka kibiashara na kutamani kupeleka mazao yao kuuza nje ya nchi.


Aliwataka wasichana hao kuamka na kujiletea maendeleo wakati wakijiamini na kuthamini kazi zao kabla ya wengine hawajatambua umuhimu wao.


Mwenyekiti wa Mtandao wa wasichana wafadhiliwa na CAMFED (CAMA)Taifa Shamsa Mkurungo alisema wamefanikiwa kusaidia watoto 114,000 na kurudisha wanafunzi walioacha shule kwa kuwapa ushauri na ushuhuda.


Pia alisema wamepata mikopo 511 isiyokuwa na riba kutoka CAMFED iliyoweza kusaidia kukuza biashara zao sambamba na kupata mitaji ya kuanzisha biashara iliyosaidia ongezeko kubwa la wana CAMA katika kuanzisha biashara mwaka 2025.


Naye msichana Elina Lukindo aliyesaidiwa na CAMFED alisema dhana ya kujiamini aliyofundishwa na CAMA imemsaidia kupata nafasi ya udiwani viti maalum Kata ya Gairo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.


Mmoja wa wanufaika wa CAMA kutoka Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mzizi Mtambwa aliishukuru CAMFED kwa kuanzisha programu hiyo iliyomsaidia kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya uongozi na uchumi Bora baada ya kumuokoa kutoka kwenye sintofahanu ya kumaliza kidato cha nne baada ya kukosa wa kumsomesha hapo awali.


Mtabwa alisema kupitia misaada ya CAMA ameweza kuendeleza kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji na kuinua kutokakuwa na uhakika wa kupata sh 1000  hadi kufikia kuwa na uhakika wa sh 10,000 ya kulimia na kuajiri baadhi ya vijana na kupunguza ukosefu wa ajira.


......

No comments: