![]() |
| Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu lissu |
![]() |
| Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Justine Masejo |
Na Mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, linamshikilia mkazi wa jiji hilo, Fredrick Mbwambo ambaye ni kada wa Chadema kwa tuhuma za wizi wa fedha za mchango wa mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 28,2026 na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Justine Masejo, Mbwambo alishirikiana na wenzake kukusanya fedha hizo zilizochangwa kwa ajili ya Lissu kupitia kampeni ya 'Funga mwaka na Tundu Lissu'.
" Ukamataji huo ulifanyika baada ya kupokea malalamiko ya Alute Mughwai ambaye ni kaka yake Lissu, baada ya kubaini wizi wa fedha hizo," amesema Masejo.
Kamanda Masejo amesema ufuatiliaji wa awali umeonyesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za kampuni tofauti ya simu inadaiwa zilihamishiwa kwenye namba mbili za simu moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ni kampuni ya simu ya nchi jirani.
Aidha, Jeshi la Polisi linawasaka watuhumiwa wanaotuhumiwa kuhusika katika wizi huo pamoja na vielelezo unaendelea ili hatua za kisheria zifuate.


No comments:
Post a Comment