Na,Queen Lema Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuhakikisha waTanzania wanapata huduma Bora za afya kupitia program ya tiba mkoba ambayo imesaisia waTanzania wengi kupatiwa huduma za kibingwa na bobezibkwa kusogezewa huduma mahali walipo.
Mkude ameyasema hayo Leo wakati alipotembelea kambi maalum ya matibabu ya Mkoa wa Arusha inayoendelea katika hospitali ya Arusha Lutherani Medical Center ALMC iliyopo jijini Arusha ambapo amemshukuru pia mkurugenzi wa JKCI kwa kutambua kusogeza huduma hiyo katika Mkoa wa Arusha hususani Wilaya ya Arusha mjini huku ukizingia Mkoa wa Arusha kuwa ni kitovu cha Utalii.
Amesema kuwa magonjwa yasiyoyakuambukiza ni moja wapo ya changamoto kubwa za kiafya duniani ambapo takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa magonjwa hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa bifo na mzigo wa kiafya katika jamii nyingi.
Ameongeza kwa kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa wote ili waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi kwani bima hiyo ni nguzo muhimu katika kufanikisha lengo la afya kwa wote.
"Takwimu za shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa vifo Milioni 17.5 sawa na asilimia 32 ya vifo vyote duniani husabanishwa na magonjwa ya moyo huku takwimu za nchini zikionyesha Mkoa wa Arusha watu wengi kuwa na matatizi mbalimbali ya kiafya ikiwemo magonjwa yasiyoyakuambukiza."Alisema Mkude
Ameongeza kuwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ni hospitali maalum ya kitaifa katika masuala ya matibabu ya moyo na kwasasa imejikita katika hospitali ya Arusha ALMC ambayo kwa sasa inasimamiwa na JKCI.
Amebainisha kuwa tangu kuanza kwa kambi hiyo Hadi Leo januari 4 ,2026 wananchi waliohudhuria ni zaidi ya 800 ikijumuisha watu wazima zaidi ya 70 na watoto 100 ambao ni wastani wa wagonjwa 155 Hadi 200 kwa siku huku vipimo vikubwa vikifanyika.
Sambamba na hayo kambi hiyo imewezesha kubaini wagonjwa wa ushauri,tiba na upasuaji wa moyo ikihusisha watu wazima na watoto pamoja na kuongeza uelewa wa huduma za JKCI na ALMC Hali iliyoweka msingi wa rufaa endelevu na uwepo wa huduma za JKCI katika hospitali ya ALMC kwa kipindi kinacho cha miaka 20 ambapo muunganiko huo ni muhimu ikizingatiwa Taifa linahitaji kuandaa mashindano makubwa ya AFCON mwakani.


No comments:
Post a Comment