MEYA MAXIMILIAN: Madiwani simamieni usafi kwenye kata zenu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 4 January 2026

MEYA MAXIMILIAN: Madiwani simamieni usafi kwenye kata zenu




 Na Queen Lema Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Meya Wa Jiji la Arusha Maximilian Iraqhe amewataka madiwani wa jiji la Arusha kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo suala la usafi kwenye kata zao pamoja na kuwachukulia hatua Kali wachafuzi wa mazingira


Kwa sasa bado zipo kata ambazo zina uchafu pamoja na mazingira yake kuwa katika hali ya uchafu mkubwa ambapo ili hali hiyo iweze kuepukika viongozi ngazi ya kata wanatakiwa kuwajibika.



Iraqhe aliyasema leo katika kampeni ya ngarisha usafi iliofanyika katika soko la mbauda kata ya sombetini


Alisema kuwa suala la usafi kwa jiji la Arusha ni lazima na wala sio Ombi ambapo sasa kila diwani anatakiwa kuhakikisha kuwa kata yake haiwi mfano Wa uchafu 



"Hii kampeni ni ya lazima sasa nitakushangaaa sana endapo kama utatamba mtaani alafu kwako ni kuchafu huu mwaka sio  wa kubembelezana Bali ni mwaka wa matekelezo zaidi na jiji letu lazima liwe safi muda wote"aliongeza


Wakati huo huo aliwataka maafisa afya pamoja na watendaji wa kata na vijiji kuacha tabia ya kukaaa maofisini zaidi Bali wapite kwenye makazi ya watu


"Naagiza kuanzia sasa haw  a watendaji wapo kwa ajili ya wananchi sasa maofisini huwa wanafanya nini kwa mfano nawataka wahakikishe wanashirikiana na madiwani Arusha safi inawezekana kabisa"aliongeza 


Alihitimisha kwa kuwataka wafanyabiaahara wa soko la mbauda kuweza kuzingatia usafi lakini pia Kuacha tabia ya kutupa  chupa za plastiki ovyo.


"Tujitaidi inasikitisha sana kukuta pembezoni mwa barabara kumejaa  chupa za plastiki tusichafue mazingira na niseme sheria zipo na kuanzia sasa hatua Kali sana zitachukuliwa"aliongeza.


Mwisho

No comments: