DC MKUDE AZINDUA MRADI WA KUKOPESHA BODABODA ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 15 January 2026

DC MKUDE AZINDUA MRADI WA KUKOPESHA BODABODA ARUSHA

 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Modest Mkude akizindua mradi wa kukopesha pikipiki kwa vijana wa Arusha



Na Queen Lema,Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Modest Mkude amefanikiwa  kuzindua mradi wa kukopeshana pikipiki sambamba na mkakati wa kurahisisha upatikanaji wa leseni Kwa jiji la Arusha


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkude alisema kuwa Neno  bodaboda linachukiliwa  vibaya wakati Kwa sasa Ajira za boda boda ni nyingi


 Alisema Kwa sasa boda boda wanatambulika kama maafisa usafirishaji na jamii inapaswa kuwapa heshima kubwa sana.


Alifanua kuwa kuwasaidia madereva wengi kuingia rasmi kwenye mfumo, ni lazima mpango wa kugharamia leseni kwa pamoja, ambapo waendesha bodaboda watachangia nusu ya gharama huku wadau wakilipia nusu iliyobaki. 


Katika hatua nyingine aliagiza Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kupunguza urasimu katika utoaji wa leseni, akisisitiza kuwa mafunzo ya siku moja yanatosha kwa madereva wanaoendesha kama biashara, badala ya kuwapeleka VETA kwa muda mrefu.


Pamoja na hatua hizo za kuwezesha, Mkude alisema operesheni dhidi ya pikipiki zitakazokiuka sheria zitaendelea, hasa kwa wahuni wanaosababisha fujo mitaani. Alisema dereva bodaboda anayejitambua hawezi kuhatarisha biashara yake kwa vitendo visivyo vya kistaarabu.


Kwa upande wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha, mwenyekiti wake Shwahibu Hamisi alisema umoja huo umeanza mradi wa kukopeshana pikipiki kwa kushirikiana na kampuni ya TVS, ambapo pikipiki 20 tayari zimekopeshwa kwa awamu ya kwanza kwa fedha zilizochangwa.


Kwa ujumla, mradi huu unatajwa kuwa hatua muhimu katika kuwawezesha vijana wa Arusha, kupunguza ajali barabarani na kuifanya bodaboda kuwa sekta rasmi yenye mustakabali mzuri wa kiuchumi na ajira.


Mwisho

No comments: