Mussa Juma,Maipac
maipacarusha@gmail.com
Mkuu wa mkoa wa Arusha, CPA Amos Makallah na Mkurugenzi wa CRDB, Abdulmajid Nsekela juzi wametamba kwenye mashindano ya CRDB Super CUP 2026 msimu wa tano.
Viongozi hao, walikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa timu mbili zilizochuana vikali, Makala alikuwa nahodha wa timu ya soka ya viongozi wa Serikali mkoa Arusha, huku Nsekela akiwa nahodha wa timu ya viongozi wa CRDB Bank.
Katika mchezo huo,Timu ya viongozi wa Benki ya CRDB ilishinda goli 1-0 kwa taabu wakati mchezaji bora wa mchezo huo akitangazwa kuwa ni Mkuu wa mkoa Arusha, CPA Makallah.
![]() |
Katika mchezo wa fainali ya wafanyakazi wa CRDB timu ya Ulipo Tupo ya Lake Zone ilitwaa ubingwa CRDB Super Cup msimu wa tano, baada ya kuifunga CRDB Wakala ya Central Zone 1-0 katika fainali iliyochezwa jijini Arusha.
Ushindi huo umeipa Ulipo Tupo kombe la ubingwa na kitita cha shilingi milioni 15, ambapo Kwa upande wa mpira wa pete, mvutano ulikuwa mkubwa kati ya Ulipo Tupo Queens na Popote Inatiki Queens, ambapo Ulipo Tupo Queens Central Zone iliibuka mshindi na kujinyakulia zawadi ya shilingi milioni 11.
Akizungumza baada ya fainali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amosi Makallah, alisema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kukuza uchumi wa mkoa huo na sehemu ya maandalizi ya AFCON 2027.
Makallah alisema mkoa wa Arusha utakuwa mwenyeji wa AFCON 2027 na wanatarajia kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi.
"Walichofanya CRDB leo ni kuanza kuhamasisha michezo mkoa Arusha na tuone kuna fursa kubwa inakuja hivyo tujiandae"alisema
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema benki hiyo itaendelea kuwekeza kwenye michezo kwa maendeleo ya jamii.
Alisema CRDB ambayo pia inadhamini michezo mbalimbali inathamani sana michezo kama fursa ya kuichumi.
Aliwataka wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutumia huduma mbalimbali za CRDB ili kukuza uchumi wao.
Katika michuano hiyo ambayo iliambatana na burudani za muziki,vyakula na michezo mengine maelfu ya wakazi wa Arusha walijitokeza
Mwisho





No comments:
Post a Comment