Dkt Mwigulu: Rais Samia ametimiza ahadi ajira 12,000 za walimu, madaktari - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 23 January 2026

Dkt Mwigulu: Rais Samia ametimiza ahadi ajira 12,000 za walimu, madaktari

 


Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya ajira za walimu 7,000 aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.


Katika mikutano yake ya kampeni za mikoa mbalimbali Dkt Samia aliahidi ndani ya siku 100 kutoa ajira 12,000 za elimu na kada ya afya.


Dk Mwigulu ameeleza hayo leo Ijumaa, Januari 23,2026 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza ambapo alipata fursa ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi vituo vya kusukuma maji jijini humo.


“Mheshimiwa Rais (Dkt Samia) alisema ndani ya siku 100 wataajiriwa walimu 7,000 tayari wameshaajiriwa na wanakwenda katika shule za sekondari mpya zaidi ya 1,300,” ameeleza Dkt Mwigulu na kuongeza kuwa 


“Wanakwenda pia katika shule za msingi mpya zaidi ya 2,700. Tayari walimu hao wapya wameshapangiwa maeneo yao ya kazi,” amesisitiza Dkt Mwigulu.


Dkt Mwigulu amesisitiza hakuna ahadi hata moja iliyoahidiwa na Dkt Samia ambayo haijatekelezwa, akifafanua kuwa hata ile ya watalaamu wa afya 5,000 imeshatekelezwa.


“Hivi tunavyoongea watalaamu hao 5,000 wameshaajiriwa ili kuwatibu Watanzania katika hospitali mbalimbali. Walisema kutakuwa na Bima ya Afya kwa Wote, leo hii shughuli inaendelea,” amefafanua Dkt Mwigulu.

No comments: