WIZARA YA AFYA YAWATAKA WADAU WA KEMIKALI KUTOA MAONI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 23 January 2026

WIZARA YA AFYA YAWATAKA WADAU WA KEMIKALI KUTOA MAONI

 




Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


WIZARA ya Afya imewataka wadau wa kemikali nchini kutoa mapendekezo kwa serikali jinsi ya kudhibiti kemikali hatarishi katika jamii.


Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt Seif Shekalaghe ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa jukwaa la kitaifa la wadau wa kemikali .


Katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa kwa niaba yake  na Mkurugenzi wa huduma za tiba wa wizara ya  afya Dkt Hamad Nyembeha, alisema mapendekezo ya wadau kwa serikali yatasaidia kwenye maboresho ya sekta ya kemikali.


"Jukwaa hili linakutanisha wadau wote wa sekta ya kemikali kuanzia watengenezaji, wasafishaji, watunzaji mpaka mtumiaji wa mwisho hivyo ni vyema wakajadili na kutoa mapendekezo kwa serikali namna bora ya kuboresha sekta hii ili kulinda afya yajamii na mazingira "alisema Dkt Shekalaghe.


Alisema sekta ya kemikali inazidi kukua hivyo ni muhimu kuwekewa mazingira wezeshi kwa kuzingatia usalama wa afya ya jamii, utunzaji wa mazingira na usalama wa nchi.


Katibu Mkuu aliongeza kuwa pia kemikali hizo zinatikiwa kutumika kuendesha shughuli za uzalishaji kwa njia salama ili zisitumike kwenye madawa ya kulevya au kutumika kama silaha hatarishi.


Dkt Shekalaghe alisema kemikali ni muhimu katika maisha ya kila siku kwani katika sekta ya vya inahitajika ili kuokoa maisha ya mgonjwa, sekta ya kilimo katika uzalishaji wa mbolea sekta ya madini katika uchenjuaji na viwandani kwa ajili ya uzalishaji 


Mkemia Mkuu wa serikali Dkt Fidelice Mafumiko alisema jukwaa la wadau jukumu lake ni kujadili, kutoa mapendekezo na kuishauri serikali namna bora ya kukabiliana na changamoto za sekta ya kemikali na jinsi ya kudhibiti kemikali hatarishi.


Mwisho.

No comments: