Dkt Samia aahidi Serikali kulinda, kuheshimu uhuru wa mahakama - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 13 January 2026

Dkt Samia aahidi Serikali kulinda, kuheshimu uhuru wa mahakama





Na mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameahidi Serikali kuendelea kulinda na kuheshimu uhuru wa mahakama ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Januari 13, 2026 akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA), uliofanyika viwanja vya makao makuu Mahakama mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu ya utawala bora na msingi wa upatikanaji wa haki kwa Watanzania.

Hata hivyo, Rais Dkt Samia ametoa rai kuhusu suala la uhuru wa mhimili huo kuwa hauna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu, nidhamu, utii wa sheria na uzalendo kwa Taifa la Tanzania.


“Hakuna Taifa linaloweza kuwa na maendeleo endelevu na ustawi wa watu wake bila usimamizi mzuri wake haki.Watanzania wana matumaini makubwa sana wangependa kuaona mahakama inayosimamia haki kwa uwazi kwa kuzingatia misingi ya kikatiba sheria na utu,” ameeleza.

Ameongeza kuwa, “Kuna mtu anafungwa kwa kesi ya kubambikiwa, sasa ‘engineering’ gani imepita mahakamani hadi mtu anafungwa kwa kesi ya kubambikiwa,”


No comments: