Mbunge Monduli asaidia Wanafunzi 200 wa Jamii za kifugaji kwenda Shule - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 14 January 2026

Mbunge Monduli asaidia Wanafunzi 200 wa Jamii za kifugaji kwenda Shule





Mussa Juma,maipac


maipacarusha@gmail.com.


Monduli. Mbunge wa Jimbo la Monduli mkoa Arusha, Izaki Joseph Copriano maarufu kwa jina la Kadogoo ametoa msaada wa vifaa vya shule na nauli kwa wanafunzi 200 kutoka kaya duni wengi wao wakiwa kutoka jamii ya kifugaji katika jimbo hilo.


Kadogoo ambaye ametangaza kipaumbele chake cha kwanza katika jimbo hilo ni Elimu, ametoa magododo 35,000 Masanduku[tranker)20,000 na nauli kwa watoto waliopangiwa shule za mbali.


Akizungumza na maipac baada ya kutoa misaada hiyo, Kadogoo amesema ameamua kuwasaidia watoto ambao wazazi  wao wanahali duni ya kiuchumi ili watoto wao waende shule.


"Kama unavyojua wilaya yetu ni wilaya ya wafugaji na suala elimu ni changamoto kubwa hivyo mwaka huu nimeanza na msaada huu na ntaendelea kushirikiana na  serikali na wazazi kutatua kero katika sekta ya elimu Monduli"amesema


Amesema ameto msaada huo pia kwa kuzingatia wilaya hiyo ipo katika  kipindi cha ukame na  jamii ya Maasai wana hali mbaya Mifungo.


"Maisha yetu Monduli asilimia 90 tunategemea mifugo hivyo kama kuna shida ya malisho ina maana uchumi wetu umekuwa mgumu sana"amesema.


Hata hivyo, Mbunge huyo amesema msaada huo bado hautoshi na akatoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kusaidia sekta mbalimbali wilaya ya Monduli.


Kabla ya kuwa Mbunge wa jimbo la Monduli, alikuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli kwa miaka zaidi ya mitano ambapo pia aliweza kushirikiana na wadau mbalimbali kuchochea maendeleo ya wikaya hiyo.


Miongoni mwa wadau hao ni Taasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) ambapo alizindua mradi wa kusaidia ujenzi wa uzio wa chanzo cha maji kijiji cha Selela wilaya ya Monduli, mradi uliodhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania kupitia programu ya miradi midogo ya mfuko wa mazingira duniani (GEF).


Mratibu wa miradi midogo ya UNDP, Tanzania Faustine Ninga alitembelea mradi huo na kuukabidhi kwa Kamati ya Mazingira ya kijiji cha Selela na kueleza kuridhishwa na mradi huo  wa kimkakati na kueleza wataendelea kusaidia  miradi inayogusa  maisha ya wananchi.


Kutokana na mradi huo ,MAIPAC  inatarajia kuboresha mfumo wa usambazaji maji kutoka chanzo cha maji cha Kabambe ambacho kimewekewa uzio na hivyo maji kuongezeka  ili maji yawafikie wananchi kwa matumizi ya majumbani, Kilimo na Uvuvi.


Mwisho.

No comments: