Dkt Samia: Kilichofanyika leo kitapongezwa na Umoja wa Mataifa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 29 January 2026

Dkt Samia: Kilichofanyika leo kitapongezwa na Umoja wa Mataifa

 





Na Mwandishi Wetu, maipac


maipacarusha20@gmail.com


Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) umetekeleza lengo namba nne kwenye malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG’S).


Dkt Samia amesema hayo Alhamisi Januari 29,2026 akizindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Darasa la I na II.


Kwa mujibu wa Dkt Samia, lengo hilo namba nne linahimiza kufanya ubora wa elimu


“Tumetekeleza mikakati yetu ndani ya Taifa, ndani ya Afrika, lakini pia kimataifa. Kwa hiyo Umoja wa Mataifa wakijua tulichokifanya leo watatupa pongezi nyingi sana, kwa haya tulioyafanya,”


“Ndugu zangu niseme, tupo katika njia sahihi na tunakwenda vizuri,” amesema Dkt Samia.

No comments: