KAMATI YA USHAURI WA KISHERIA WILAYA YA MTWARA YAJIPANGA KUENDERLEA KUWAHUDUMIA WANANCHI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 22 January 2026

KAMATI YA USHAURI WA KISHERIA WILAYA YA MTWARA YAJIPANGA KUENDERLEA KUWAHUDUMIA WANANCHI





Na mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Kamati ya ushauri wa kisheria wilaya ya Mtwara, imekutana katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika leo tarehe 22 Januri 2026 Mjini Mtwara, kikiwa na lengo la kufanya majadiliano kuhusiana na majukumu ya kamati,kupanga mikakati ya utelezaji na kujenga misingi ya ushirikiano kati ya kamati na wadau wengine katika kutoa ushauri wa kisheria.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za ushauri wa kisheria za mkoa, ambaye pia ni wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara Nunu Mangu, amesema wajumbe wa kamati hiyo wameaminiwa na kupewa jukumu la kipekee la kusaidia ushauri na uangalizi katika utekelezajiwa wa huduma za ushauri wa kisheria na elimu ya sharia kwa wanaanchi wa wilaya ya Mtwara.


“Kamati hii imeundwa kwa mujibu wa sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Utekelezaji wa Majukumu) Huduma za Ushauri wa Kisheria za Mikoa na Wilaya, Vidokezo vya mwaka, 2024)”


“lengo kuu la kamati hii ni kuwawezesha Mawakili wa Serikali kuhakikisha utawala wa sharia unafuatwa na kutekelezwa katika Mikoa na Wilaya kwa minajili ya kupunguza migogoro ya kisheria dhidi ya serikali na kutoa hudumaza ushauri wa kisheria kwa viongozi katika ngazi ya wilaya na wananchi kwa ujumla” ameeleza Wakili nunu Mangu.


Pia amewataka wajumbe kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kushughulikia malalamiko ambayo yatapokelewa kwenye kamati zao sambamba na kuhakikisha kuwa vikao vya kamati vinakaliwa kwa wakati katika kila robo mwaka na kuwasilisha taarifa kwa kamati ya mkoa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ushauri wa kisheria wilaya ya Mtwara, Wakili mfawadhi wa ofisi ya wakili mkuu wa Serikali Mtwara Thomas Mahushi, ameipongeza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa kuwezesha uanzishwaji wa kamati hizo ambazo amesema zitaleta tija kubwa katika sekta ya sharia nchini.


Naye mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Wakili wa Serikali Wakili kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Vivian Swai, amesema kuwa uanzishwaji wa kamati hiyo unaenda kusogeza huduma msaada wakisheria kwa wananchi.


“kama alivyosema mwenyekiti kamati hizi zinalenga kutoa msaada wa kisheria kwa wanachi bure, kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wote wenye uhitaji huo wanafikiwa na msaada huu bila kutoa malipo yoyote” amesema


No comments: