![]() |
![]() |
Na Lilian Kasenene,Pwani.
maipacarusha20@gmail.com
SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na utoaji elimu ya Umeme kwa wateja wake juu ya masuala mbalimbali na taratibu za namna mteja anavyoweza kupata umeme.
Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mafia Pwani kusini Fortidas Ishabairu, akiwa ameambatana na timu kutoka Ofisi ya Uhusiano Tanesco Mkoa wa Pwani kusini, alisema Dhumuni la elimu hiyo kwa wananchi ni kujenga uelewa juu ya Miradi Mipya iliyijengwa na Tanesco pamona na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
"Wateja wetu tutawaeleza majukumu na tofauti kati ya REA na Tanesco namna wanavyoshabihiana," alisema Ishabairu.
Akieleza na kutoa Elimu kwa wananchi wa vijiji vya Juani na Jibondo alisema Wateja Wana haki ya kupata umeme kwa kufuata taratibu kama kufanya maombi kupitia mfumo wa Nikonekt na njia nyingine nne kama tulivyozieleza ikiwemo masuala ya usalama, ulinzi na miundombinu.
Kaimu meneja huyo alisema njia nyingine ni kuhusu Nishati safi, Hali ya upatikanaji umeme kwa Sasa na hali inavyoendelea ya kuboresha mfumo wa Nikonect.
Alizungumzia suala la usalama aliwataka kuhakikisha wanazingatia usalama na kutofanya shughuli za kijamii chini ya miundombinu ya umeme, kuzingatia mita tano, kutumia wakandarasi wenye leseni za EWURA, namna ya kupata wakandarasi, kuwaripoti vishoka na wale wanaojihusisha na kuomba wateja rushwa akiwaasa wananchi kitojihusisha na rushwa.
"Shirika linaendelea na kuboresha na kufanya matengenezo kinga ili kuboresha Hali ya upatikanaji umeme, tunaendelea na mradi kwa ajili ya kuondoka changamoto"alisema.
Wenyeviti wa vijiji vya Juani na Jibondo waliishukuru Serikali kwa kuona na kuthamini umuhimu wananchi kupata umeme katika visiwa hivyo kupata Nishati ya umeme.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Juani Mwichande Bakari aliahidi kupokea na kuendelea kulinda miundombinu na kushirikiana na Serikali pamoja na Tanesco.
Nae mwenyekiti wa Kijiji cha Jibondo Hassani Amri Mohamedi alipongeza Serikali,Shirika la Tanesco na akasisitiza kuzingatiwa kwa yake yote waliyoelimishwa na wataalamu.
Mwisho .


No comments:
Post a Comment