Wakulima 500 Handeni kunufaika na mbegu za mbaazi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 26 January 2026

Wakulima 500 Handeni kunufaika na mbegu za mbaazi





Burhani Yakub,Handeni.

maipacarudha20@gmail.com


Zaidi ya wakulima 500 wa Wilayani Handeni wanatarajiwa kunufaika kwa kugawiwa mbegu ya mbaazi itakayozalishwa na wakulima watakaopewa mafunzo ya uzalishaji wa mbegumama.


Mbegu hizo zinatokana na mbegumama iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko (COPRA) na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.


Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hizo yaliyofanyika katika soko la wakulima wa nafaka Mbweni lililopo Kijiji Cha Mkata Afisa Kilimo kutoka Copra Kanda ya Kaskazini,Paskalia Sitembela amesema zoezi hilo lipo katika mpango wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima.


Amesema kupitia mpango huo Copra imetoa mbegu mama za mbaazi kilo 300 katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za saraja iliyoazimiwa la (QDS) kwa vijana na chama cha ushirika cha MVIWATA.


"Ugawaji wa mbegu ni utaratibu wa serikali wa kurejesha sehemu ya tozo ya mauzo ya mazao kwa wakulima waliouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabdhi ghalani ambapo wakulima wa mkoa wa Tanga na wilaya ya handeni ni miongoni mwao"amesema Paskalia.


Jumla ya kilo 300 za mbegu mama za mbaazi aina komboa imekabidhidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya uzalishaji mbegu bora àmbapo kilo sita aina hii zinatosha kuoteshwa kwenye ekari moja ikipandwa kila shina punje mbili.


Mbegu hizi kwa mujibu wa maelezo ya afisa huyo zinakomaa kati ya miezi minne hadi sita na mavuno yake ni kati ya tani moja hadi mbili kwa ekari moja.


Mkuu wa divisheni ya Kilimo,mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,Yibalila Chiza amesema kuanzia wiki ijayo wakulima wateule wataanza kupokea mafunzo ya namna bora ya uzalishaji wa mbegumama Ili ziweze kusambazwa kwa wakulima.


Akizungumza baaada ya kupokea mbegu hizo,Afisa Tarafa ya Mazingara,Mnyamisi Msilagi amewaagiza maafisa ugani kusimamia vyema uzalishaji wa mbegu hizo Ili zilete tija kwa wakulima.




"Ikiwa kwa awamu ya kwanza tu kilo 300 mbegumama zitazalisha kati ya tani 70 na tisini ni wazi kuwa baadaye idadi ya wanufaika 500 itaongezeka mara dufu...tuwasimamie wakulima wazalishe kwa ubora unaotarajiwa"amesema Msilagi.


Mwanaidi Mhanganwela ambaye ni mkulima kutoka chama cha ushirika cha Mviwata ameahidi kutumia mafunzo atakayopewa kuzakisha mbegu bora ya mbaazi.


MWISHO

No comments: