![]() |
| WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewaondoa wasiwasi wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ya wanyama, viumbe maji na nyanda za malisho kuwa hawatapoteza kitu chochote kutakana na uwepo wa fursa za kutosha kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Balozi Dkt Bashiru alisema hayo alipokutana na wanafunzi wa shahada ya kwanza nyanda za malisho waliokuwa kwenye masomo kwa vitendo ya upandaji wa malisho ya mifugo kwenye shamba darasa la chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA alipofanya ziara ya siku Moja Chuo hapo.
Katika ziara hiyo pia alipata fursa ya kuzungumza na wataalamu wa SUA na wakurugenzi wa taasisi za Mifugo na Uvuvi zilizochini ya Wizara hiyo.
Amesema bila ya malisho huwezi kufuga kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayolazisha kuweka msisitizo mkubwa kwenye uzalishaji wa malisho kwasababu nyasi za asli katika nyanda za malisho yameanza kupiteza sifa kutoka na ukame wa mda mrefu na wafugaji wengi kupoteza mifugo
“Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ni moja ya vyuo vyenye heshima katika nchi yetu katika masuala ya mafunzo, ushauri wa kitaalamu na utafiti kwenye kilimo, mifugo, uvuvi na misitu na mimi kilichonileta hapa ni mambo mawili mifugo na uvuvi”. Amesema
Waziri alisema kutokana na ukame huo wafugaji wa mikoa ya Manyara, Singida, Simiyu, Tabora na Mara
Dkt. Bashiru amesema Wizara yake imepewa maelekezo na Rais pamoja na dira ya maendeleo ya taifa 2050 imewaelekeza kuhama kutoka kufuga kienyeji na kufuga kisasa yenye tija ufanisi na kwamba wanafunzi watumie vizuri masomo wanayoyasoma kwa kufanya utafiti na baadae kwenda mtaani watafanya mambo ya maana kwani eneo hilo la malisho ni biashara kubwa na waliochangamkia wameanza kufanikiwa.
” Mnayoyasoma hapa msidhani mnapoteza muda hili eneo la malisho sasa litakuwa ni biashara kubwa na waliochangamkia wamenza kupata biashara hiyo. Kuna biaashara ya mbege zake, biashara ya malisho yenyewe na nyinyi hapa mnafundishwa namna ya kuyasindika ili kuyaongezea thamani nawapongezeni sana kwa kuchagua kusoma katika eneo hili muhimu kwenye mifugo”. Amesema
Waziri huyo alisema amebaliana na uongozi wa Chuo kikuu SUA kwa kutengeneza kamati ya kutoka wizarani na chuo hicho ambayo itasimamiwa na ofisi yake pamoja na SUA ili ziweze kuwaongoza kwenye maeneo ya utafiti, mafunzo na ushauri wa kitaalamu hasa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, mabwawa, malisho na maabara.
”Nimetembea maabara na nimejionea ilivyo ya kisasa ambayo inaviwango vya kimataifa”.
Akizungumza na watendaji wa wizara hiyo pamoja menejimenti ya SUA amesema bado kuna ufa mkubwa wa kimahusiano na kiutendaji baina ya Wizara hiyo na taasisi zake ambao unatakiwa kuzibwa na njia pekee ni kuwa na ushirikiano.
Alisema mchango wa sekta ya mifugo na Uvuvi hauridhishi ukilinganisha na rasilimali zilizopo, Mifugo ni nafuu lakini kwa Uvuvi ni kidogo wakati lasilimali za Uvuvi ni nyingi ukilinganisha na nchi nyingi za ukanda wa Afrika mashariki.
Akizungumza katika ziara hiyo Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael Chibunda amesema pamoja na kuwa na changamoto ya bajeti waliyonayo lakini chuo kimekuwa kikitenga shilingi Bilioni 1 kwaajili ya kufanya utafiti hasa kwenye kujenga watafiti wapya kwa sababu ya ushindani wa soko la kupata fedha za utafiti kuwa mdogo.
Alisema mpango huo umezaa utunda na hivyo ameiomba wizara na taasisi kuwa na utaratibu wa kutenga fedha kwaajili ya kuendeleza utafiti hasa kwa watafiti wapya.
Mwisho



No comments:
Post a Comment