Na mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Serikali kupitia Wakala wa nishati vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 203 kutekeleza miradi saba ya kusambaza nishati ya umeme kwenye vijijini na vitongoji mkoani wa Mtwara, katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.
Miradi hiyo ni pamoja na REA 3 ROUND 2 uliaanza mwaka 2021 ukiwa na thamani ya Shilingi bilioni 98, uliokuwa na lengo kuhakikishakuwa Viviji vyote 785 vya mkoa wa Mtwara vinafikiwa na umeme, ambao ulitekelezwa katika Wilaya zote za mkoa huo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Safari Radio-Mtwara tarehe 29 Januari 2026, Msimamizi wa miradi ya REA katika mkoa wa Mtwara, Mhandisi Daniel Mwandupe ameutaja Mradi wa pili wenye thamani ya Shilingi bilioni 56, ambao ulilenga kufikisha umeme katika Vitongoji 451. Mradi huu unaitwa Ujazilizi 2C.
Mhandisi Daniel ameeleza kuwa Mradi wa tatuambao ulishakalimika ulikuwa wa kufikisha umeme katika Migodi, na maeneo ya kilimo ukiwa na thamani ya shilingi Bilioni 3.5, ili kuhakikisha kwamba Migodi midogomidogo inatumia nishati salama katika matumizi yake ambapo jumla ya migodi 13 katika Mkoa wa mtwara .
“Mradi wa nne pia ulishakamilika,ulikuwa wa kufikisha umeme katika vituo vya Afya na vyanzo vya maji wenye thamani ya shilingi bilioni 3.35, ambao ulikuwa na lengo la kukabiliana na changamoto za magonjwa ya Uvico (Covid 19) na vituo vya afya na vyanzo vya maji 18 vilifikiwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.35"
"Mradi wa tano unalenga kufikisha umeme katika vitongoji 150 katika majimbo yote 10 ya mkoa wa Mtwara kwa kila jimbo kunufaika na vitongoji 15,unatarajiwa kukamilika septemba 2026, thamani yake ikiwa ni shilingi bilioni 16.7" ameeleza . Mradi huu unaitwa Mradi wa HEP 2A
Aidha ameuelezea Mradi wa sita uliolenga kusambaza umeme maeneo ya pembezoni mwa miji, katika maeneo ya miji yenye hadhi inayofanana na vijiji uliogharimu shilingi Bilioni 11.25, ambao ulizifikia Halmashauri za Mtwara mikindani, Mtwara DC, Newala na Masasi na kunufaisha maeneo au mitaa yenye hadhi ya vijiji yapatayo 41. Mradi huu unaitwa Peri-Urban III
Mradi wa 7 ni HEP 2B unaolenga kufikisha umeme katika vitongoji 175, ambao Makandadari wake alitambulishwa kwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara tarehe 28 Januari 2026 utakaogharimu kiasi cha fedha shilingi bilioni 15.3 na unatarajiwa kunufaisha kaya 5,646. Mradi huu unaitwa HEP 2B.
Mkoa wa mtwara una jumla ya Vijiji 785 ambavyo vyote vimefikiwa na umeme kupitia wakala wa nishati vijijini (REA), na vitongoji 3,421 ambavyo katika yake ni vitongoji 520 pekee ambavyo havijafikiwa na huduma ya umeme, huku serikali ikiwa na mpango wa kuhakikisha kuwa vitonghoji vyote vinafikiwa na umeme ifikapo mwaka 2030.


No comments:
Post a Comment