DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAJI SINYA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 23 February 2026

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAJI SINYA.






 Na mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 23, 2026 amekagua maendeleo ya Mradi wa Majisafi wa Sinya–Namanga unaotekelezwa eneo la Sinya, Longido mkoani Arusha.


Mradi huo unaotarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji hadi lita 4,100,000 kwa siku, unatekelezwa na mkandarasi M/s. Zongii Contractors Co. LTD kwa gharama ya Shilingi bilioni 13.5 ambazo zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Mradi huo unategemea kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Namanga na Sinya kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maji ambayo chanzo cha sasa cha Mto Simba hakitoshelezi. 


Maji yatakayo toka katika mradi huo ambao hadi kufikia Januari 2026 ulikuwa umefikia asilimia 24.7 yatakidhi mahitaji ya wananchi na mifugo.

No comments: