TFS YAJIONGEZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI,YAFIKIA WATALII LAKI 346 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 23 February 2026

TFS YAJIONGEZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI,YAFIKIA WATALII LAKI 346

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


KATIBU mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Hassan Abasi amesema Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) imeonyesha kwa kujiongeza kwenye shughuli za kiuchumi ambapo kwa Mwaka 2024/2025 imeweza kufikia watalii 346,000 kutoka watalii sifuri.


Amesema hayo wakati akifunga mkutano mkuu wa nne wa mwaka wa makamanda wa Kanda Saba wa wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS,wahifadhi wakuu wa Wilaya, wa mashamba,hifadhi wa Misitu ya Mazingira asilia na vituo vya Mali kale nchini.


Dk Abas alisema miaka kadhaa ya nyuma TFS haikuwa na shughuli zozote za Utalii lakini kwa Sasa imekuwa ya mfano kwa kuziongezea Wizara Pato ambapo aliwataka kuendelea kujihimarisha katika shughuli nyingine za kiuchumi.


"Kwa Sasa mmeona kuwa hii ni shughuli lasmi ya kuziongezea kipato, si tu kuleta watalii mfano katika maduhuli Mwaka 2025  mlipanga kukusanya shilingi bilioni 176 lakini mlipanda hadi kufikia sh 189 bilioni mwisho wa Mwaka," alisema.


Alisema kwa Mwaka huu mpaka 2026 Juni waliweka makadilio ambayo mpaka kufikia Februari imekusanya kiasi cha sh Bilioni 127, sawa na asilimia 70.


Aidha katibu mkuu huyo aliongeza kuwa,kwa ujumla wake TFS imeweza kusaidia mauzo kuongezeka katika soko la nje ambapo kwa takwimubmauzo ya nje Tani za asili Mwaka Jana zilizouzwa ni 1,596 yenye thamani ya sh bilioni 19.2 na Nta bili 2.9.


"Kwa ujumla wake mauzo nje ya nje yamefikia sh Bilioni 196.98 hongereni kwa usimamizi, mchango wa sekta ya Misitu na nyuki kwenye pato la Taifa Sasa imefikia asilimia 3.5," alisema Dk Abasi.


Katibu mkuu huyo akaipongeza TFS  kwa kutoa mchango katika sekta hiyo ya uhifadhi wa Misitu, kwani imesimama kidete licha ya changamoto za kiutendaji zilizopo katika kulinda Misitu 464, mashamba 24 na mashamba ya nyuki 3.


Pia alisema pamoja na Wizara kuwa na jukumu la kutoa mchango katika kustahimilisha mifumo ikolojia na kulinda baionuai, Makamanda wa TFS Wana jukumu la kustawisha misitu kwa maendeleo ya nchi na dunia kwa jumla.


Akawakumbusha makamanda hao kuwa Wizara  ni mojawapo ya Wizara za Kimkakati zenye jukumu la kutoa mchango mkubwa katika kustahimilisha mifumo ikolojia na kulinda baionuai hivyo makamanda wana jukumu la kulinda na kustawisha misitu kwani ni sekta nyeti sana kwa maendeleo ya nchi.


"Tunapotimiza wajibu wetu vizuri tunazisaidia sekta nyingine kukua kama mnavyofahamu dunia inapambana kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu (17 Sustainable Development Goals adopted by the General Assembly of the United Nations). 


Akizungumzia kwa niaba ya menejimenti, Kamishana wa Uhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo  alisema mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa kada mbalimbali wakiwemo makamanda wa kanda, wahifadhi wakuu wa wilaya, maafisa na askari, kwa lengo la kujenga uwezo wa kiuongozi, maadili na ufanisi wa kiutendaji.


Profesa Silayo alisema TFS imeendelea kupata mafanikio yanayotambulika ndani na nje ya nchi zikiwemo tuzo katika sekta ya uhifadhi na utalii, huku mkutano huo ukijikita pia katika fursa za utalii ikolojia, afya ya akili, nidhamu ya kazi, na mapambano dhidi ya rushwa na uzembe.


“Utalii ikolojia kwenye misitu ni eneo lenye fursa kubwa ya mapato na ajira. Tunaamini TFS itakuwa mdau muhimu katika kufikia lengo la Taifa la watalii milioni nane ifikapo 2030,” alisema Profesa Silayo.


Kaulimbiu katika mkutano huo One Team, One Dream.


Prof.Silayo alisema katika mkutano huo walipata bahati ya kupata mihadhara kutoka kwa wabobezi kwenye maeneo mbalimbali kama 

Huduma kwa mteja, itifaki na Ustaarabu (Protocol),

mwelekeo wa utalii ikolojia (Opportunities, Challenges and Way Forward in Ecotourism).


Maeneo mengine waliopitia ni Afya ya akili, magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza (Mental health, communicable and non-communicable diseases),

Kujitambua (Self Awareness)

Elimu kuhusu utakatishaji fedha (Anti money laundering)  

Mrejesho kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa tatu wa TFS 

kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na changamoto kutoka katika vituo mbalimbali. 


Mwisho.

No comments: