Dkt. Samia ateta na viongozi mbalimbali ziarani Dubai - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 3 February 2026

Dkt. Samia ateta na viongozi mbalimbali ziarani Dubai

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kossovo, Vjosa Osmani-Sadriu, kabla ya kufanya vikao na viongozi mbalimbali pembezoni mwa mkutano wa Jukwaa la Serikali za Dunia (WGS2026), leo 3 Februari, 2026 Madinat Jumeirah, Dubai, Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE).


Na mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Leo Jumanne, Februari 3, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameanza ziara ya kikazi nchini Dubai, UAE kwa kufanya mazungumzo na viongozi na wadau wa kimataifa. 


Katika ratiba ya leo, Rais Samia anakutana na Gaston Browne, Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda, pamoja na kufanya mazungumzo ya pande mbili na Shaikha Al Nuwais, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano, diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja nchini. 


Jioni ya leo, Rais Samia atashiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) — jukwaa la uwekezaji linalolenga kuoanisha miradi iliyo tayari kuwekezeka barani Afrika na wawekezaji wa kimataifa. GAIS ni mpango wa kimkakati unaoendeshwa sambamba na majadiliano ya sera ya World Governments Summit (WGS), kwa lengo la kubadili majadiliano ya sera kuwa uwekezaji halisi wenye matokeo.

No comments: