Dkt Samia: Tuepuke vitendo vinavyovunja heshima ya jeshi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 24 February 2026

Dkt Samia: Tuepuke vitendo vinavyovunja heshima ya jeshi




Na mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuishi kwa misingi ya viapo vyao, akiwasisitiza kuepuka vitendo vinavyovunja heshima ya jeshi hilo.


Dkt Samia ameyasema hayo jijini Dodoma leo, Jumanne Februari 24, 2026 wakati wa hotuba yake, baada ya unziduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.


“Utii kwa mamlaka ya kikatiba na uaminifu kwa Taifa, ndio silaha ya kwanza ya jeshi linaloheshimika, hivyo niwasihi muendelee kuishi kwa misingi ya kiapo chenu na kuepuke mienendo inayoweza kuharibu heshima ya jeshi letu,” amesema.


Amenukuu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yanayosema, “moyo kabla ya silaha” akifafanua yanafundisha msingi wa jeshi imara ni uzalendo, nidhamu, weledi, utii na dhamira safi, uadilifu na uaminifu wa askari wake kwa Taifa na watu wake.

No comments: