Na mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema hatua ya kukua kwa uchumi wa Taifa na maendeleo yanayoshuhudiwa ni matokeo ya kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama nchini na kwamba hata ustawi wa wananchi hauwezekani bila amani.
Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Februari 24, 2026 alipohutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dodoma.
“Juzi tu shirika la kimataifa linalofanya tathmini ya ukuaji wa hali ya uchumi duniani the Moody’s limeipa nchi yetu daraja la B1, ambalo ni kiwango kizuri kwa mustakabali wa ukuaji wa uchumi wetu,” amesema.
Amesema kila nchi inapokua kiuchumi, uwekezaji katika sekta ya ulinzi ni suala lisiloepukika kutokana na umuhimu wake kwa mustakabali wa Taifa, maendeleo na ustawi wa wananchi.

No comments:
Post a Comment