Na mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ameeleza namna walivyokubaliana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuhusu kuimarisha shughuli za usafiri na usafirishaji baina ya mataifa hayo mawili.
Rais Samia ametoa kauli leo Jumamosi Februari 7,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam, akiwa na mgeni wake, Rais Museveni wakizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.
" Kama mnavyojua nchi zetu ambazo hazina bahari wanategemea sana bandari za Tanzania, tumezungumza namna watakavyopata nafasi ya kuzitumia bandari hizi ili kusafirisha mizigo," amesema Dkt Samia.
![]() |
Na kuongeza kuwa," Kubwa zaidi niwewapa taarifa kuwa Tanzania ndani ya ilani ya CCM- 2025/30 tuna nia ya kujenga reli itakayounganisha Tanga hadi Musoma na huko mizigo itasafirishwa wa ziwa Victoria hadi Uganda jambo lililowapa faraja," ameeleza Dkt Samia.



No comments:
Post a Comment