MKULIMA ADAIWA KUVAMIA ENEO LA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 7 February 2026

MKULIMA ADAIWA KUVAMIA ENEO LA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI

 



Na  Mwandishi wetu,Manyara


maipacarusha20@gmail.com


 BAADHI ya wakazi wa  kijiji cha Laghandamur kata ya Bargish Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wamelalamikia uvamizi wa ardhi uliofanywa  kwa nguvu na Doday Qwari  kwa kujenga nyumba ya bati sita katika eneo lisilokuwa lake. 


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Charles Longo ambaye ndio mmiliki wa eneo hilo lililovamiwa ameema kuwa  eneo hilo la zaidi ya ekari tatu anamiliki   yeye kihalali kisha badae aliuza ekari moja kwa serikali ya kijiji cha Laghandamur kwaajili ya  kujenga zahanati ya kijiji


Lakini chakushangaza alifika katika eneo hilo lililokuwa wazi ambalo si lake na kujenga nyumba ya bati Sita katika shamba hilo na kudai ni lake lakini uhalisia eneo hilo ni langu na hati miliki ya eneo hilo ni MT/316/08 ambayo inasomeka kwa jina langu


"Suala hili nimelifikisha polisi, kwa viongozi mbalimbali sijapata msaada na sielewi huyu Doday anapata kiburi gani kuvamia eneo langu na eneo ambalo kijiji niliwauzia ili wajenge zahanati yeye kaenda kujenga eneo si lake naomba msaada wa eneo langu alilochukua na la kijiji arudishe na yeye atafute pa kwenda kwani amevamia na analima eneo si lake"


Longo amesema kwa sasa anashindwa kulima eneo  hilo lililovamiwa ambalo ndilo eneo hilo wanalitegemea kwaaajili ya kilimo na kukuza shughuli za uchumi wa familia hivyo aliomba uongozi husika haswa idara ya ardhi kushughulikia changamoto hiyo ili aweze kuendelea na majukumu ya kilimo 


Naye Mwenyekiti wa serikali katika kijiji hicho, Raphael Tluwai alikiri kuwepo kwa mgogoro huo uliopelekea zahanati ya kijiji kishindwa kujengwa kutokana na uvamizi wa eneo hilo uliofanywa na  Doday hivyo kutokana na mgogoro huo laiupeleka ofisi ya ardhi na kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ili kupata utatuzi wake lakini hadi leo hii mgogoro huo  haujapata ufumbuzi wake. 


"Ni kweli sisi kijiji tumeuziwa eneo la ndugu Charles lakini huyu Doday sijui anapata wapi kiburi kaja kujenga eneo ambalo si lake na sasa hivi sisi kama uongozi wa kijiji tunapeleka suala hili baraza la ardhi kata ili kupata suluhu ya utatuzi wa changamoto hii ili kila mtu abaki katika mipaka yake na hapa katika eneo hili tulilonunua na kupanga kujengwa zahanati basi tujenge au tuazimie kujenga mradi mwingine lakini mgogoro huu uishe kwanza "


Hata hivyo Doday alipopigiwa simu ili kujua kwanini amejenga eneo linalodaiwa si lake amesema eneo hilo anajua ni lake ila hajui ukubwa wake ndio maana amejenga nyumba ya much inayoweza kubomolewa endapo wahusika kutoka idara ya ardhi katika Wilaya ya hiyo wafike kupima ili kubaini mipaka halisi ya eneo hilo na kuondoa taharuki kati ya uongozi wa kijiji, kwa Charles

No comments: