Serikali kuongeza mikopo ya halmashauri hadi asilimia 15 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 6 February 2026

Serikali kuongeza mikopo ya halmashauri hadi asilimia 15

 


Na Mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepanga kuongeza mikopo ya halmashauri kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu, kutoka asilimia 10 hadi 15, utakapoanza mwaka ujao wa fedha 2026/27.


Hatua hiyo inalenga kutanua wigo wa wananchi wa makundi hayo watakaonufaika na mikopo hiyo, inayotokana na sehemu ya mapato ghafi ya halmashauri, manispaa na majiji nchini.


Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo, Alhamisi Februari 5, 2026 na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, alipohutubia wakati wa hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh200 bilioni kwa ajili ya uwezeshaji vijana na wanawake.


Amesema kiwango hicho cha asilimia zitakazoongezwa, kinalenga kutumika kutengeneza mazingira wezeshi zaidi ya biashara hasa kujenga miundombinu kama masoko na maeneo ya makundi hayo kufanyia biashara.


“Dkt Samia ameshaelekeza kwamba kwenye kundi la vijana, wanawake na wenye ulemavu waliokuwa wanapata mgawo kupitia mapato ya ndani ya halmashauri, kwamba ifikapo Juni baada ya mwaka mpya wa fedha kuanza, Serikali inakusudia kuongeza asilimia nyingine tano kwa ajili ya makundi haya ikiwa ni mahususi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu,” amesema.

No comments: