![]() |
| Eva Mwambungu (capacity building officer THRDC) akiendesha mjadala pamoja na maswali na majibu katika mafunzo hayo |
Mwandishi wetu,Arusha.
maipacarusha20@gmail.com
Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu Tanzania(THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za asili(MAIPAC),imeanza kuwanoa wanahabari Kanda ya Kaskazini na Kati, kuandika vyema Habari za uchunguzi za mazingira.
Uzinduzi wa mafunzo hayo, umefanyika leo Februari 5,2026 jijini Arusha, kwa kushirikisha waandishi 35 kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Tanga, Singida, Manyara na Dodoma na yanadhaminiwa na shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO).
![]() |
| Mkurugenzi wa programu na uendeshaji wa THRDC, Wakili Halima Sonda akifungua .afunzo hayo mapema leo |
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa programu na uendeshaji wa THRDC, Wakili Halima Sonda, alisema wanahabari wanajukumu kubwa la kuhakikisha dunia na wananchi wanakuwa salama.
Wakili Sonda alisema Dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira, hivyo wanahabari wanajukumu la kuokoa dunia na wananchi.
“lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wanahabari kuandika vyema Habari za mazingira, uchafuzi mazingira, ukataji miti na uchimbaji holela wa madini”alisema.
![]() |
| Mussa Juma Mkurugenzi Maipac akiwasilisha mada |
Akitoa mada juu ya uandishi wa Habari za mazingira katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa MAIPAC,Mussa Juma alisema ni muhimu wanahabari kujikita kuandika vyema Habari za mazingira kwani zina mahusiano makubwa na haki za binaadamu.
Juma alisema THRDC na MAIPAC inakusudia kutoa mafunzo kwa wanahabari 140 nchi nzima kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi, ukataji miti, uchafuzi wa mazingira, kudhibiti taka ngumu na masuala ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori na sheria mbalimbali za mazingira na ardhi.
“Baada ya mafunzo haya tunaimani tutakuwa na timu ya waandishi waliobobea katika masuala ya uandishi wa mazingira”alisema.
Juma alisema kuna Habari nyingi zinahitaji uchunguzi, ikiwepo umuhimu matumizi ya nishati safi na kuachana na kukata miji, uvamizi wa watu maeneo ya jamii za asili kama Wahadzabe na kufungua mashamba,uchimbaji holela wa migodi na matumizi ya kemikali zenye madhara, kusagaa kwa taka ngumu.
![]() |
| Wakili Paulo Kisabo akiwasilisha mada kwa wanahabari wa mazingira kanda ya kaskazini |
Akitoa mada ya sheria mbali mbali za ardhi, mazingira na Habari, Wakili Paulo Kisabo alisema, masuala ya mazingira yanauhusiano mkubwa na haki za binaadamu.
Kisabo alikumbusha wanahabari sheria mbali mbali za kimataifa na ndani ya nchi kuhusiana na masuala ya haki za binaadamu, mazingira na uhuru wa kujieleza.
“Wanahabari fanyeji kazi kwa kuzingatia sheria,mnalindwa na sheria nyingi za ndani na hivyo mkitumia vizuri kalamu zenu mtalisaidia sana taifa”alisema
Wakili Kisabo,alisema ni muhimu wanahabari kujua sheria mbali mbali kwa manufaa yao kwani kujifunza sheria sio kwa wanasheria pekee.
Mafunzo hayo, yanaendelea jijini Arusha na baadae yatafanyika katika kanda nyingine hapa nchini.
![]() |
MWISHO.












No comments:
Post a Comment