Mahakama zaongezwa Tanga - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 5 February 2026

Mahakama zaongezwa Tanga







Burhani Yakub,Tanga.


maipacarusha20@gmail.com


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Katalina Mteule amesema huduma za mahakama Mkoani Tanga zimesogezwa kwa wananchi baada ya kuongezwa mbili na hivyo kufikia 69.


Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini amesema kutokana na mahitaji kuongezeka mahakama mpya zilizojenga ni ya Kilole Wilayani Korogwe na Msomera iliyopo Wilaya ya Handeni.


Jaji Mteule ambaye pia alikagua gwaride la askari wa kikosi cha kutuliza ghasia cha jeshi la polisi amesema ongezeko hilo la mahakama ni katika jitihada za kuondoa mrumdikano wa mashauri mahakamani.


Awali Mahakama za mwanzo mkoani Tanga idadi yake ilikuwa 67 na baada ya kujengwa nyingine mbili zimefikia 69 huku mahakama za Wilaya zikiwa nane,Mahakama ya Hakimu Mfawidhi pamoja na mahakama kuu Kanda ya Tanga.


Amesema siku chache zijazo mahakama hiyo itapata jengo jipya la Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kutokana na jengo lililopo kuzidi kuwa kongwe huku mahitaji yakiendelea kukua.


" Kutokana na ukongwe wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na jengo letu limekuwa kongwe ...siku si nyingi zijazo tutapata jengo jipya la Mahakama Kuu Kanda ya Tanga litakalokidhi mahitaji ya sasa na siku za mbele"amesema Jaji Mteule.


Jaji huyo pia amesema katika kukabiliana na kasiya mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya sasa ya utoaji huduma mfumo wa kompyuta umeondoa rushwa naa urasimu uliokuwa ukilalamikiwa zamani.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dr Batilda Burian amesema changamoto ya migogoro ya ardhi katika maeneo mengi mkoani hapo bado ipo na kwamba ofisi yake inajitahidi kuyapatia suluhu kabla ya kufikishwa mahakamani.


"Tatizo ni kwamba wengi wa wananchi hawana elimu ya mirathi hawaelewi ni michakato ipi ifuatwe baada ya kuteuliwa kusimamia mirathi"amesema Dr Batilda Burian.


Hata hivyo amesema huduma ya elimu na utatuzi wa migogoro iliyoendeshwa na Mama Samia Regal Aid ni iliweza kusaidia kutatua migogoro mingi ya ardhi iliyokuwa sugu.


"Mama Samia Regal Aid imewezesha kuwajengea uwezo wa kisheria pamoja na kutoa msaada wa kisheria ikiwamo kutatua migogoro iliyokuwa sugu mkoani Tanga.


Amesema Serikali mkoani Tanga ina mpango wa kutafuta ardhi na kutoa kwa Mahakama,jeshi la polisi na Chama cha Mawaikili wa kujitegemea (TLS).


Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoa wa Tanga,Rebecca Msalangi amesema ongezeko la majaji,mahakimu na Mawaikili,kupungua kwa msongamano wa mashauri mahakamani na katika mabaraza mbalimbali na matumizi ya kisasa ya kupokea,kuhifadhi na kutoa taarifa kumerahisisha kumaliza haraka mashauri.


Ametaja mambo yanayotekelezwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa ni pamoja na upekuzi wa mikataba amabo umesaidia kuhakikisha inatekelezeka na inazingatia misingi yote ya sheria.


Katika mwaka wa fedha 2024/25 jumla ya mikataba 3436 na hati makubaliano 729 zilifanyiwa upekuzi na Mwasheria Mkuu wa Serikali.


Amesema ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanya maboresho na ufasili wa sheria mbalimbali ambao umesaidia kupatq rejea za sheria kirahisi ambapo mwaka wa fedha 2024/25 miswada 16 ya sheria iliandaliwa sheria ndogo 1018 ziliandaliwa huku sheria 446 zilifanyiwa urekebu.


Mwenyekiti wa chama cha Mawakili wa kujitegemea (TLS) mkoa wa Tanga,Mary Swai amesema kwa kushirikiana na vyombo vya dola wameanza kupambana na vishoka wa sheria.


"TLS mkoa wa Tanga tumeanza kampeni ya kuwasaka vishoka wa sheria ambao wanaendesha shughuli za kisheria halafu wanawatelekeza njiapanda wananchi...tunashirikiana na vyombo vya dola katika kampeni hii"amesema Swai.


MWISHO

No comments: