Chem Chem na Chair the love watoa msaada viti mwendo Babati. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 30 March 2026

Chem Chem na Chair the love watoa msaada viti mwendo Babati.









Mwakilishi wa shirika la Chair of Love,Glen Mather alisema wamekuwa wakitoa misaada kwa Jamii Tanzania ili kutambua mchango wao wa uhifadhi wa mazingira.                         
   


 

Mwandishi wetu,Babati.


maipacarusha20@gmail.com 


 Taasisi ya Chem Chem iliyowekeza shughuli za Utalii wilayani Babati, mkoani Manyara kwa kushirikiana   Shirika la Chair The Love kutoka Nchini Marekani wametoa msaada wa viti mwendo 148 kwa wananchi wenye uhitaji wilaya ya Babati.


Msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia jamii ambayo imekuwa ikitolewa na Chem Chem wilayani Babati katika sekta ya Afya, Elimu, Maji na huduma nyingine za kijamii.


Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu 


Akizungumza  wakati wa kukabidhi viti hivyo, Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu alisema wanapongeza shirika la  Chair The Love la Marekani kuendelea kushirikiana na Chem Chem katika kusaidia jamii.


Zulu aliwataka wananchi waliopo katika vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi ya wanyamapori ya jamii ya Burunge, eneo ambalo taasisi hiyo  imewekeza kuendelea kutunza mazingira na wanyamapori ili kuendelea kuvutia watalii zaidi.


Meneja Miradi ya maendeleo ya jamii wa Chem Chem, Napendael Wazoeli


Meneja Miradi ya maendeleo ya jamii wa Chem Chem, Napendael Wazoeli alisema  Lengo  la Chem Chem ni kuisaidia Jamii kupitia uhifadhi ambao umeendelea kuwanufaisha Wananchi ambao wapo pembezoni mwa hifadhi.


Wazoeli alisema, msaada huo ni sehemu ya matunda ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori katika wilaya hiyo ambayo Chem Chem imewekeza Utalii wa picha na hoteli.


Mwakilishi wa shirika la Chair of Love, Glen Mather alisema wamekuwa wakitoa misaada kwa Jamii Tanzania ili kutambua mchango wao wa uhifadhi wa mazingira. 

  
  Mather alisema pia wameona kuna uhitaji wa kusaidia watu wenye matatizo ya kutembelea.      "Tutaendelea kushirikiana na Chem Chem kusaidia jamii ili kila mmoja afurahie maisha yake"alisema


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, Mwanasheria wa Halmashauri  hiyo Jofrey Jaffar amewataka Jamii kuendelea kuunga Mkono Taasisi ya Chem Chem ambayo imewekeza katika wilaya hiyo ili kuendelea kunufaika.


Jaffar alisema taasisi ambazo zimeweleza katika eneo hilo la Burunge WMA zimekuwa zinaigusa jamii moja kwa moja kupitia misaada inayotolewa.


Baadhi ya wananchi waliopokea msaada huo waliishukuru  Taasisi  ya Chem Chem  na washirika wake kwa msaada huo ambao utarahisisha maisha yao.


Rehema Peter mkazi wa kijiji cha Vilima vitatu moja ya vijiji 10 vinavyounda hifadhi hiyo aliomba Taasisi hizo kuendelea kutoa msaada kwa wahitaji ambao bado hawajafikiwa kwa njia moja ama nyingine. 


Msaada huo umetolewa kwa mwaka wa nne sasa na Taasisi ya Chem Chem kwa ushirikiano na Shirika la Chair The Love kutoka Nchini Marekani ambao wameahidi kuendelea kusaidia kwenye maeneo mbali mbali hapa Nchini.



Mwisho.

No comments: