Jamii yatakiwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote kwa wakati - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 31 March 2026

Jamii yatakiwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote kwa wakati

 



Na: Queen Lema,Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Wito umetolewa Kwa jamii kuhakikisha kuwa chanjo zote zilioorodheshwa  na wizara ya afya zinatekelezwa ipasavyo hasa kwa watoto na kuachana na tabia ya kuruka au kuacha  chanjo kikamilifu


Yapo madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa watoto endapo kama wazazi au walezi watakwepa chanjo ambazo zimeelekezwa Kwa mujibu wa 


Akizungumza leo tarehe 30,Machi,2026  Jijini Arusha wakati wa Mafunzo kwa Viongozi Wasimamizi Huduma za Chanjo (Mid-level Managers - Training on Immunization Services MLM)  yaliyowahusisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga, Afisa Afya kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, Wizara ya Afya, Bw. Bonaventura Nestory amesema kuwa uzingatiaji wa ratiba za chanjo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata kinga kamili kwa wakati sahihi.


Nestory alisema kuwa kwa sasa Serikali imeweza kupambana na chanjo Kwa asilimia 98 hivyo jamiii inapaswa kuhakikisha watoto wote wanapata huduma ya afya kama vile mpango wa taifa unavyoelekeza



Mbali na hayo pia alizitaka nazo halmashauri kuhakikisha kuwa zinasimamia ipasavyo mpango huo Wa chanjo ambapo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa jamii yote inanufaika na huo mpango wa chanjo kwa asilimia zote 



Naye mmoja wa washiriki WA mafunzo  hayo  Bw Japhet simeo Alisema kuwa mafunzo hasa kwenye mpango wa chanjo utawasaidia Sana kwani wataweza kuangalia  mambo mbalimbali ambayo yanakwamisha  chanjo 


Aliendelea kwa kusema kuwa pia  wataendelelea kuangalia hata namna ya kuboreshwa huduma za  chanjo Kwa kuangalia rasilimali zilizopo kwenye jamiii Kwa haraka Ili kutekeleza Yale ambayo yamekusudiwa na Serikali.


Mshiriki mwingine  ambaye ni Afisa Wa chanjo kutoka TAMISEMI,Bi Rosalia Arope alisema kuwa kuna umuimu WA washiriki kuhakikisha kuwa wanaboresha huduma zao kuanzia ngazi ya chini 


Rosalia alisema kundi Hilo la washiriki wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuatilia watoto wote waweze kupata Chanjo

No comments: