Soil for the Future Tanzania yahimiza wafugajiji Monduli na Longido kukimbilia mradi hewa ya Carbon ya Udongo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 31 March 2026

Soil for the Future Tanzania yahimiza wafugajiji Monduli na Longido kukimbilia mradi hewa ya Carbon ya Udongo

 




Na Queen Lema, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 


Wito umetolewa kwa wafugaji wa wilaya za Monduli na Longido kuhakikisha kuwa wanajumuika Kwa pamoja kwenye mradi wa hewa ya Carbon ya Udongo 


Mradi huo unaotekelezwa na Soil for the future  umeweza kutekelewa kwenye vijiji zaidi ya 15 kutoka katika wilaya za Monduli pamoja na Longido mkoani Arusha 


Akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo Bw Richard  Ndaskoi alisema kuwa mradi huo umekuwa na faida kubwa sana kwa wafugaji wa wilaya hizo 


Akitaja faida ni pamoja na kuwa na maongezeko  ya uuzaji wa Carbon lakini pia hata uhakika wa malisho ambayo yanaweza kuwanufaisha wafugaji wenyewe


"Huu mradi unasaidia sana kwa mfano hii carbon ya  udongo inatokana na mimea  michanga na mifugo inatakiwa Ile kiasi lakini ile mifugo ikishakula  Kwa kiasi inaacha inaenda sehemu nyingine ambayo  ina malisho hapo sasa mifugo inakuwa na uhakika kabisa wa malisho"aliongeza 


Katika hatua nyingine alidai kuwa wafugaji wa vijiji vya wilaya hizo mbili  wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakimbilia mradi huo kwani mbali na elimu pia wataweza kuwanusuru mifugo Yao hasa nyakati za ukame


"Ukame ulitokea wiki chache hapa Arusha lakini vijiji ambavyo vimejiunga na mradi huu mifugo Yao ilizoroteka  tu na haikufa lakini walibaki hai sasa basi nawakaribisha sana waje kwenye mradi huu' alisema 


Alisema kuwa mradi huo katika wilaya hizo mbili wameweza kutekeleza mradi huo Kwa asilimia 50 ingawaje walitamani Mpaka sasa wawe wamefikia kiwango kikubwa cha utekelezaji lakini bado wamekutana na changamoto mbalimbali 


Alitaja changamoto hiyo kuwa ni pamoja na kuwepo na baadhi ya watu wasio na nia Njema na mradi huo wa hewa ya Carbon ya Udongo.


Ndaskoi Alisema kuwa kundi Hilo la watu wamekuwa wakiwarubuni baadhi ya vijiji na kuwaaminisha kuwa hawapaswi kujiunga na mradi huo kwani wanaweza kuibiwa ardhi Yao Jambo ambalo sio la kweli kabisa


"Mimi nataka kusema kuwa huu mradi hauna nia ya kunyanganya Mtu ardhi yake Bali tunawawezesha kwa kiasi  kidogo alafu wao sasa watakuja kuzalisha wwenyewe na kuuza mapato yatarudi kwenye jamii "aliongeza

No comments: