Mwandishi wetu.
maipacarusha20@gmail.com
CHAMA cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), jana rasmi kimeanza kushiriki mkutano wa Taasisi zinazopigania Haki za kupata Habari (CoRI).
JOWUTA alipitishwa na CoRI katika kikao chake cha tatu kilichofanyika Desemba 5 mwaka jana, baada ya kutuma maombi ya kujiunga kutokana na jukumu lake kubwa la kutetea na kulinda maslahi na uhuru wa wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania.
Katika kikao cha kwanza JOWUTA, iliwakilishwa na Mwenyekiti wake wa Taifa,Mussa Juma ambaye alitumia fursa hiyo kushukuru wanachama wa CoRI kwa kukubali JOWUTA kuwa mwanachama.
Juma alisema uhuru wa kupata habari unapaswa kwenda pamoja na maslahi bora kwa wafanyakazi katika vyombo vya habari.
![]() |
| Mwenyekiti wa jowuta TaifaMussa juma |
Alisema JOWUTA itashirikiana na taasisi nyingine 22 ambazo ni mwanachama wa CoRI katika kuhimiza haki ya kupata taarifa lakini pia kupigania maslahi bora kwa wanahabari nchini.
"JOWUTA tuna wanachama zaidi ya 400 hivyo tutatoa ushirikiano unaohitajika katika kutekeleza majukumu ya CoRI lakini pia tunatarajia kunufaika na ujuzi na uzoefu wa wanachama wengine wa CoRI"alisema
Mwenyekiti wa CoRI, Ernest Sungura alitambulisha wanachama wengine wapya mbali JOWUTA waliopitishwa kujiunga na CoRI ni shirika la TAMCODE,Taasisi ya Mawakili ya Divine Elite Attorneys, RUJAT, TMC na mfuko wa vyombo vya habari (TMF)
"Tunawakaribisha CoRI tushirikiane kupigania sekta ya habari ili iweze kusonga mbele zaidi kwa pamoja,"amesema.
Katika kikao hicho ,kilichofanyika.jijini Dar es Salaam, CoRI ilipitisha mapendekezo ya sehemu ya mpango kazi mwaka 2026.
Mwisho.





No comments:
Post a Comment