![]() |
| Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete |
![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro |
![]() |
| Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete |
_📌Kamati ya Bunge yapongeza Jinsi Wizara ya Utumishi na Utawala Bora ilivyo thabiti kuteketeza miradi kwa ubora mkubwa._
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Jumanne Machi 10, 2026 Jijini Dodoma mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Waziri Kikwete amesema utekelezaji wa shughuli zilizopangwa katika kipindi hiki umefanyika kwa kuzingatia fedha zilizopatikana pamoja na muda wa upatikanaji wake kwa lengo la miradi hiyo kuongeza tija nchini lakini pia kuwa chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma huku akiishukuru na kuiahidi Kamati hiyo kuwa Ofisi anayoisimamia itaendelea kushirikiana nao katika kuimarisha na kuboresha utendaji kazi ili kuleta tija katika kuwahudumia wadau mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo nchini.
![]() |
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akiongoza kikao cha Kamati yake hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
“Kwa niaba ya Kamati yangu nitoe pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan maana ndiye mwenye ofisi hii, kwa hakika mnafanya kazi nzuri kwa kumwakilisha Mhe. Rais.” Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro
Vilevile, Mhe. Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Waziri Kikwete kwa taarifa nzuri aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo iliyoelezea kwa kina utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo itaongeza chachu ya maendeleo nchini.
Mhe. Dkt. Ndumbaro ameiahidi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kuwa itashirikiana nayo katika usimamizi wa masuala mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.
![]() |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete |





No comments:
Post a Comment