MAPENDEKEZO YA BAJETI 2026/2027 HALMASHAURI ya Wilaya ya Iramba ni shilingi billioni 47 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 11 March 2026

MAPENDEKEZO YA BAJETI 2026/2027 HALMASHAURI ya Wilaya ya Iramba ni shilingi billioni 47

 


NA: SEIF TAKAZA, IRAMBA 


maipacarusha20@gmail.com 


HALMASHAURI ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Imepitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti Ya mapato na matumizi Zaidi ya shilingi billioni 47 Ambapo ni ongezeko la bilioni 8 za mwaka uliopita ya shilingi billioni 39 


Hayo yamebainika jana katika kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo mwaka wa fedha 2026/2027 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Inosent msengi amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanahamasisha makusanyo ya mapato na tozo mbalimbali ili halmashauri hiyo iweze kikidhi utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii katika halmashauri hiyo .

Msengi amesema halmashauri hiyo kukusanya mapato ya ndani Zaidi ya shilingi billioni 4 hivyo kila diwani anapaswa kuhakikisha fedha alizopitisha kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027

“hii ni rasimu ya bajeti hivyo inatubidi tuchangie mawazo ili tuongeze mapato ya halmashauri yetu “

Aidha Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisisitiza wataalam wabuni vyanzo vya mapato vingine ili halmashauri iwe na mfuko wakutosheleza mahitaji ya wananchi au wanajamii kwa ujumla 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Samweli Asheri wakati akitoa salam za chama ameipongeza halmashauri hiyo kwa kupitisha bajeti ambayo inaweza kukidhi mipango ya maendeleo ya Wilaya hiyo .

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba Halmashauri yako iwe na utaratibu wa kufatilia vyanzo vya mapato ambapo kwa upande wa madini tozo zilizopo katika bajeti hazilingani na wenye madini hivyo inawapasa kuwa makini katika ukusanyaji wa mapato upande wa madini, kupitisha bajeti ni jambo moja lakini kusimamia shughuli za utekelezaji ni jambo jinguine, hivyo mnapaswa kuwa makini katika kutoza tozo za Madini.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kiomboi Omar Hassan alitoa ushauri kwa wanaosimamia mazao hasa vitunguu na nyanya ambapo katika kuweka ujazo hawaweki kihalali kwani wengi wao hutumia lumbesa hivyo kumfanya kumpunja mkulima na kuipunguzia halmashauri mapato.

Kikao cha halmashauri cha bajeti ya wilaya kilitanguliwa na kamati ya ushauri wa wilaya(DCC) ambacho kilifanyika juzi kupitia bajeti hiyo.


 MWISHO

No comments: