Mafuwe aishukuru serikali kwa kutoa fedha zaidi ya bilioni 6.9 kwa ajili ya miundombinu, Hai - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 21 March 2026

Mafuwe aishukuru serikali kwa kutoa fedha zaidi ya bilioni 6.9 kwa ajili ya miundombinu, Hai

 



Na Mwandishi wetu, Hai


maipacarusha20@gmail.com 


Hai.Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe, ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi bilioni 6.9 kwa ajili ya ukarabati wa barabara na madaraja katika wilaya hiyo.


Amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafirishaji na kuimarisha uchumi wa wananchi wa Jimbo la Hai.


Aidha, Mafuwe amewataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu na kuendelea kuwanufaisha kwa kuwaletea maendeleo endelevu.


Mbunge huyo ameyasema hayo leo wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara inayotekelezwa.


Mwisho.

No comments: