![]() |
Na Pamela mollel,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi zake za kuhamasisha wanawake kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hususan katika sekta za utalii na uhifadhi, hatua inayochangia kuongeza usawa wa kijinsia na kuwajengea wanawake ujasiri wa kushika nafasi za uongozi.
Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Sekela Mwangota, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Mwangota amesema uongozi wa Rais Samia umefungua fursa zaidi kwa wanawake kuamini uwezo wao, kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki kikamilifu katika maamuzi muhimu ya maendeleo ndani ya taasisi na jamii kwa ujumla.
Alitoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8, 2026 katika ukumbi wa Mafao House jijini Arusha, ambapo wanawake wa TANAPA waliungana kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwangota alisema siku hiyo ni fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya jamii,
Katika hafla hiyo iliyobeba ujumbe wa “Nguvu ya Mwanamke wa TANAPA, Fahari ya Uhifadhi na Utalii,” Mwangota alimkaribisha Mtaalamu wa Itifaki na Mwanadiplomasia Mwandamizi, Omary Kashera, kutoa mada kuhusu nafasi ya wanawake katika uongozi na maendeleo.
Kashera alisema kuwa Siku ya Wanawake Duniani ilianzishwa mwaka 1911 kwa lengo la kupigania haki na usawa wa wanawake duniani.
Alitolea mfano mafanikio ya Rais Samia kama uthibitisho kuwa mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuongoza na kushinda changamoto mbalimbali za maisha, huku akimnukuu aliyekuwa Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Michelle Obama akisisitiza kuwa wanawake wanapaswa kuendelea kujiamini na kusonga mbele licha ya changamoto wanazokutana nazo.



No comments:
Post a Comment