WADAU WA SEKTA YA MAJI WATAKIWA KUJA NA MPANGO MADHUBUTI WA USAWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 16 March 2026

WADAU WA SEKTA YA MAJI WATAKIWA KUJA NA MPANGO MADHUBUTI WA USAWA

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki amewataka watumishi wa wizara ya maji pamoja na wadau wa sekta ya maji kujadili na kuja na mpango madhubuti wa kuweka usawa katika upatikanaji wa maji kwa watu wenyew mahitaji maalum


Waziri Kairuki alitoa Rai wakati wa mdaharo wa wadau wa maji na jinsia mkoani Morogoro ikiwa ni katika  uzinduzi wa wiki ya Maji ambapo alisema kuwa mdaharo huo ni muhimu ukaenda sambamba na kujadili kundi la watu maalum ili kuwa na usawa wa pamoja


Waziri Kairuki pia alisema serikali na wadau wa maendeleo katika sekta ya maji wanatakiwa kulipa kipaumbele kundi la watu wenye mahitaji maalumu katika suala la upatikanaji wa maji badala ya kutizama kundi la wanawake na wasichana pekee.


Alisema kwa kuwa wadau wa sekta ya maji wamekutana kwenye jukwaa hilo itakuwa fulsa mahususi kuuungana na serikali kuangalia kundi hilo maalum hasa wanawake wenyewe ulemavu na wanawake ambao wanalea kaya za wenye ulemavu


"Ni vyema huko mbeleni tuje tuangalie namna ya kuhudumia watu wenye makundi maalum, tunafanyaje katika kuangazia upatikanaji wa maji tunawawekea mifumo ya namna Gani?, tukitambua kama mwanamke wa kawaida anachangamoto ya maji, iweje kwa mwanamke mwenye ulemavu? Iweje kwa mwanamke ambaye analeta familia ya wenye ulemavu," alisema Kairuki.


Katibu mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri alisema wizara imejipanga vizuri katika kuhakikisha maoni yanayotolewa na wadau katika mdahalo huo yanapokelewa na kufanyiwa kazi kadri itakavyowekekana


Alisema mdahalo huo imeandaliwa maalum kwaajili ya kuwaweka pamoja wadau ili kujadili nafasi ya jinsia katika upatikanaji wa maji Safi na usafi wa mazingira pamoja na uhifadhi ,usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji


"Mdahalo huu unatumika kama jukwaa la kujadili mikakati ya kuboresha sera, mipango na ushirikiano wa wadau kuhakikisha huduma za maji zinapatikana kwa usawa na uendelevu wa jamii yote," alisema.


Naye mwakilishi wa mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la WaterAids Christina Mhando,  alisema shirika hilo linaamini maji sio tu huduma bali ni njia ya kufungua milango ya usawa wa kijinsia katika jamii.


Alisema jamii zinazopata huduma Bora ya maji, wanawake na wasichana ambao wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa linapokuja suala la upatikanaji wa maji maisha yao hubadirika na wanapata afya Bora, muda na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii


"Tumekuwa tunaweka kipaumbele Cha usawa wa kijinsia katika miradi tunayotekeleza ikiwemo ya maji kwa kutambua kwamba uwekezaji katika huduma za maji si tu suruhisho la kiufundi Bali ni kichocheo Cha haki, heshima na mabadiliko ya kitabia,"alisema.


Mwisho.

No comments: