WAZIRI WILLIAM LUKUVI AFARIKI DUNIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 25 March 2026

WAZIRI WILLIAM LUKUVI AFARIKI DUNIA




Mheshimiwa William Lukuvi enzi za uhai wake






Na mwandishi Wetu




maipacarusha20@gmail.com




Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kwa masikitiko kifo cha Mbunge wa Jimbo la Isimani na aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, William Vangimembe Lukuvi, kilichotokea leo Machi 25, 2026 jijini Dodoma




Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotilewa na na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses M. Kusiluka, imesema Lukuvi amefariki dunia majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa marehemu alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na kifo chake ni pigo kubwa kwa serikali na wananchi wa Jimbo la Isimani.

Rais Samia ametoa pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na Watanzania wote kwa msiba huo mzito.

No comments: