BALTON TANZANIA watua Iringa wazindua viuatilifu kusaidia wakulima. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 23 April 2026

BALTON TANZANIA watua Iringa wazindua viuatilifu kusaidia wakulima.






Meneja Mkuu wa Kampuni ya Balton Tanzania, Jacob Vorster







Mwandishi wetu, Iringa.


maipacarusha20@gmail.com 


 Kampuni ya pembejeo za kilimo nchini, ya Balton Tanzania Ltd imewafikia wakulima wa Iringa baada ya kuzindua viualtilifu vya aina 10 ili kuwasaidia wakulima kupambana na wadudu na kudhibiti magugu


Meneja Mkuu wa Kampuni ya Balton Tanzania, Jacob Vorster akizungumza katika uzinduzi huo jana April 22, 2026 mjini Iringa alisema kampuni hiyo imebuni bidhaa hizo mpya za viuatilifu vya kulimo vilivyotengnezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ili kudhibiti wadudu na magugu kwa ufanisi na kuwasaidia wakulima kwenye mazao yao.


Vorster akizungumza na mawakala wa pembejeo za kilimo wa Mkoa huo aliwataka kuanza kusambaza viuatilifu hivyo kwa wakulima wa mazao mbalimbali ili waongeze uzalishaji.


Alisema ulinzi wa mazao ni jambo la Muhimu kwa wakulima ili wapate tija kwenye kilimo ndiyo maana KAMPUNI ya Balton Tanzania imekuja na utatuzi wa changamoto ya wadudu kwa wakulima.

"Ni muhimu sana wakulima kulinda mazao kwasababu wasipolinda yataliwa na wadudu na watapata mavuno kidogo sana" alisema Vorster

Mtafiti wa Viuatilifu kutoka Balton Tanzania, Wema Chonya


Kwa upande wake Mtafiti wa Viuatilifu kutoka Balton Tanzania, Wema Chonya alisema kutokana na changamoto ya Mabadiliko ya Tabianchi Kampuni hiyo ipo kwaajili ya kuwasaidia wakulima kuhusu matumizi Bora ya viuatilifu kwenye mazao yao.


Aidha alisema wanazingatia ubora wa bidhaa hizo ili Mkulima anapotumia aweze kuinuka na kuwa na uchumi mzuri.


"Kampuni ya Balton Tanzania inataka Mkulima akinunua bidhaa kwetu iwapo amelima ekari Moja basi mwaka unaofuata alime ekari tatu Hadi Tano" Alisema Chonya

Samwel Gambalela, Bwana shamba wa Mkoa wa Mbeya na Songwe kutoka Kampuni ya Bulton Tanzania



Samwel Gambalela ni Bwana shamba wa Mkoa wa Mbeya na Songwe kutoka Kampuni ya Bulton Tanzania, alisema wamekuwa wakiwatembelea mawakala na wauzaji wa pembejeo ili kuhakikisha wanatoa elimu sahihi kwa wakulima juu ya matumizi ya bidhaa hizo.




Nao baadhi ya mawakala kutoka Mkoa wa Iringa wamesema ujio wa bidhaa hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya kuharibika kwa mazao ya wakulima na kueleza kuwa wamekuwa wakiwaelimisha wakulima matumizi ya viuatilifu kulingana na aina ya mazao.

No comments: