
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Yusuph Mwenda akiwasisha taarifa ya Utekelezaji ya Ilani ya CCM Januari -Disemba 2025
NASEIF TAKAZA – IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
HALMASHAURI Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi Wilayani Iramba, Mkoa wa Singida imepokea taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya uchaguzi 2025 – 2030 ambayo imewasilishwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Yusuph Mwenda.
Kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM kimefanyika juzi katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Iramba Mjini hapa.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo Suleiman Mwenda ameeleza kuwa yamepatikana mafanikio makubwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya kilimo, elimu, afya, miundombinu, uvuvi, maji na umeme pamoja na ukusanyaji wa mapato
“Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokuwa nimekuja Wilaya hapa mwaka 2021 mapato ya TRA yalikuwa milioni 800 ambapo kwa sasa TRA imekusanya takribani bilioni tano lengo la ukusanyaji lilikuwa 3,500,000,000/= na kwa upande wa Halmashauri hii ina lengo la kukusanya 3,213,000/= hadi kufikia mwezi Disemba mwaka jana imekusanya milioni 163,712,000/=” alisema DC Mwenda.
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema Wilaya ya Iramba inakusaidia kujenga shule za sekondari nne na Serikali inakusudia kujenga Chuo kikuu cha Mzumbe, na wataalamu wamekuja Wilayani kuangalia sehemu Chuo hicho kitakapo chengwa.
Hata hivyo Mwenda amekipongeza Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Samweli Joel Asheri kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati na amesisitiza kuwepo na mshikamano ili Wilaya iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Hali kadhalika Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa watendaji na wadau wote wa maendeleo kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato na kusimamia miradi ya maendeleo, lakini pia alisema kuhusu vijana wachangamkie fursa mbalimbali ikiwemo madini ambapo amesema vijana wengi hawana leseni za kuchimba madini na kupewa mikopo na serikali ili kukuza na kuendeleza uchumi wao na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Samwel Ashari, amempongeza DC Mwenda kwa kuiwasilisha taarifa hiyo namna nzuri ya uwasilishaji, amesema tuzidi kuwaombea Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano Dr Samia Suluhu Hassan na Mbunge wetu Dr Mwigulu Lameck Nchemba ambaye ni waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Itakuwa ni aibu endapo tutashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutimiza wajibu wetu mahali ambapo Waziri Mkuu anatoka tuonyeshe mfano na wenzetu wajifunze kwetu hivyo tutakapofanya vizuri itakuwa ni faraja kwake” alisisitiza Mwenyekiti Asheri
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu Gyole Kiula alisema ni vizuri kuilinda miradi yetu ili vizazi vijavyo viweze kuendelea kutumia.
“Ni wajibu wetu hasa sisi vijana kuhakikisha tunakuwa watulivu na kufanya kazi kwa bidii halikadhalika kudumisha amani ya nchi yetu kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa” alisema Gyole.
MWISHO
No comments:
Post a Comment