FADev yawafundisha wachimbaji madini usalama - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 25 April 2026

FADev yawafundisha wachimbaji madini usalama




Burhani Yakub Tanga


Wachimbaji wa madini ya ujenzi wa Jijini Tanga wameiomba Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo (FADev) kuongeza zaidi mafunzo ya usalama ili waweze kupata uelewa wa namna ya kujikinga na hatari wawapo mgodini.


Wametoa ombi hilo leo walipokuwa katika mafunzo kwa vitendo ya utambuzi wa viashiria vya hatari yaliyofanyika katika mgodi wa mawe ya ujenzi uliopo Kiomoni Jijini Tanga na kuendeshwa na maafisa kutoka shirika la FADev kwa kushirikiana na wataalamu wa Tume ya Madini.


Mwanamkasi Rasi amesema katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili yeye na wachimbaji wenzake wadogo wameweza kupata uelewa wa masuala mengi ikiwamo kutambua viashiria vya hatari wawapo mgodini na kujikinga,kuendesha uchimbaji kibiashara na uchimbaji wenye kuhifadhi mazingira.


"Kabla ya mafunzo haya tulikuwa tukifanya kazi katika mazingira hatarishi mno kila siku wachimbaji na waponda kokoto walikuwa wakipata kizunguzungu kwa sababu ya kutojua namna ya kujikinga na jua kali...kupitia mafunzo haya tumepewa mbinu ambayo ni salama zaidi"amesema Mwanamkasi.


Idd Kuziwa ambaye pia ni mjumbe wa chama Cha wachimba madini (Tarema) mkoa wa Tanga kuna haja ya kupata mafunzo ya kina zaidi kuhusu utambuzi wa viashiria vya hatari vya hatari mgodini ili waweze kufanya kazi wakiwa katika usalama.


"Tumekunaliana kuwaailisha ombi letu kwa uongozi wa FADev ili katika programu zao za mafunzo walizotupangia hapa mgodini waongeze yawe endelevu tunadhani yatatujengea uwezo wa kuendesha uchimbaji ulio salama zaidi,utakaotutajirisha huku tukitunza mazingira"amesema Kuziwa.


Afisa programu wa FADev,Rehema Mkuli amesema mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) yakiwa na lengo la kuendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa.madini ya ujenzi wa Kiomoni ili watambulike kuwa wana mchango mkubwa katika sekta ya madini lakini pia ni kuwajengea uwezo wa kuongeza stadi za maisha.


"Dhima yetu ni kukuza uchimbaji mdogo wa madini unaowajibika na endelevu ikiwa ni pamoja na kuongeza stadi za maisha miongoni mwa wadogo wa madini.... lakini dira yetu ni kuhakikisha kwamba shughuli za sekta ya uchimbaji mdogo wa madini nchini Tanzania ni adilifu, shirikishi na endelevu"amesema Rehema.


Mhandisi uchenjuaji madini wa Tume ya Madini, Jackson Shirima amesema wachimbaji wengi hufanya kazi bila kuchukua tahadhari wakati kuna baadhi ya majanga yanakwepeka kwa kuzingatia viashiria.


"Kwa kuzingatia hilo Tume ya Madini kwa kushirikiana na FADev tumewapa mafunzo kwa vitendo ya kuangalia viashiria vya hatari na kuchukua hatua ya kujihami"amesema Shirima.


MWISHO

No comments: