JENGENI UTAMADUNI WA KUJISOMEA-Shkh Dr Abdulrazaq - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 25 April 2026

JENGENI UTAMADUNI WA KUJISOMEA-Shkh Dr Abdulrazaq

 


Watanzania wametakiwa kujijengea utamaduni wa kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali kama njia mojawapo ya kujipatia maarifa.


Aidha imeelezwa kuwa ni katika kujisomea pekee Watanzania watajiongezea uelewa wa masuala mbalimbali ya Dunia na Akhera yao na hasa katika dunia hii ya _utandawazi._


Wito huo umetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Cha Ahlul Bayti(ABC) Cha jijini Arusha Sheikh Dr Abdulrazaq Ameir Juma wakati akizungumza katika mahojiano maalum na maipac blog.


Sheikh Dr Abdulrazaq ambaye ni Msomi wa Elimu ya Dini, Mhadhiri wa Kimataifa, Mwalimu mtaalam wa Elimu ya Maendeleo ya Jamii na mwandishi wa Vitabu amesema maarifa mengi kwasasa yamefichwa katika maandishi.


Sheikh Dr Abdulrazaq ambaye ni mshindi wa Tuzo Maalum za Mh Mufti wa Tanzania katika Uandishi wa vitabu, amesema uvivu wa kujisomea vitabu na machapisho mbalimbali miongoni mwa wanajamii kunawanyima maarifa mengi ambayo yanapatikana katika maandishi.


Amewasihi Watanzania kutumia vizuri fursa hii ya utandawazi kwa kujifunza mambo anuwai yanayotokea katika ulimwengu ili wasije kupitwa na wakati.


Akizungumzi Tuzo Maalum ya Mufti aliyoipokea mwishoni mwa mwaka jana jijini Dar Es Salaam,Sheikh Dr Abdulrazaq amesema ameipokea Kwa heshma kubwa na kwamba imempa ari kubwa ya kuendelea kuandika kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.


Katika hatua nyingine Sheikh Dr Abdulrazaq Ameir Juma ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania,amewataka Watanzania kuendelea kudumisha  amani ambayo ni tunu ya Taifa letu.


Amesema Amani ni moja ya nyenzo muhimu za maendeleo na bila Amani hakuna fursa ya kupata maendeleo kama ambavyo ameandika katika moja ya vitabu vyake *Amani Yetu Maendeleo Yetu.*


Vitabu vingine ambavyo vimeandikwa na Sheikh Dr Abdulrazaq na ambavyo vinapatikana katika maduka mbalimbali ya vitabu ni  *Amani Kwa Mtazamo wa Uislam* na *Uhalisia  Wa Utandawazi.*

No comments: