![]() |
| Mwanasheria mkuu wa Serikali Hamza Johari |
Na Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mwanasheria mkuu wa Serikali Hamza Johari amewataka watumishi wa ofisi yake pamoja na wadau wengine wa sheria kuhakikisha kuwa wanaisoma vyema Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 na kuielewa ipasavyo kwani ofisi yake inatakiwa kutekeleza Dira hiyo kwa asilimia zote
Mbali na kuisoma na kuielewa ipasavyo Dira hiyo pia wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii zote
Mwanasheria huyo ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akizungumza kwenye baraza la wafanyakazi wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali mapema leo.
Johari alisema kuwa dira ya mwaka 2050 ya maendeleo inalenga kuinua taifa lakini pia ili dira hiyo iweze kuwanufaisha sekta ya sheria inatakiwa kila mmoja aweze kuzisimamia ipasavyo
"Dira ya 2050 sisi ni washiriki tena wakubwa natumia jukwaa hili kuwahimiza kila mmoja aisome aielewe lakini pia muhakikishe kuwa mnawajibika ipasavyo kwenye masuala ya sheria"aliongeza.
![]() |
| Wanasheria wa Serikali |
Wakati huo huo aliwataka wafanyakazi wa ofisi hiyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia malengo ya ofisi.
"Malengo yetu pamoja na vipaumbele tulivyoweka kama Taasisi vinatakiwa kufanyiwa kazi kila kazi nzuri tunayoifanya kwa kushirikiana inaruhusu hata ongezeko kubwa la bajeti ya ofisi yetu" aliongeza
Naye Mwenyekiti wa Tughe ,Baraza la wafanyakazi ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Rashid Kigalu, alisema kuwa wao kama watumishi wa ofisi hiyo wanashukuru Ofisi yao kwa kuweza kuwapa fursa mbalimbali kama vile mafunzo Sekta ya Afya,pamoja na mafunzo ya ndani ya uwajibikaji wao
Kigalu alisema kuwa fursa hizo zimeweza kuruhusu uwajibikaji wa hali ya juu hali ambayo imeleta hata ongezeko kubwa la bajeti ya ofisi hiyo.



No comments:
Post a Comment