MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI ATOA MITAJI KWA VIONGOZI WA MATAWI BAGAMOYO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 15 April 2026

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI ATOA MITAJI KWA VIONGOZI WA MATAWI BAGAMOYO

 




Na Julieth Mkireri MAIPAC Bagamoyo



maipacarusha20@gmail.com 



MWENYEKITI Jumuiya ya Wazazi kata ya Zinga Pascal Njoroge ametoa mitaji kwa matawi ya Jumuiya hiyo kuwezesha kujitegemea na kuwainua kiuchumi.


Njoroge ametoa mitaji hiyo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi zake alizoziweka wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka mmoja uliopita.


Akizungumza April 14 katika tawi la Mlingotini alipokutana na baadhi ya viongozi wa matawi ya Kondo na Mlingotini alisema mitaji hiyo ni kwa ajili ya kuanzisha biashara za kuwaingizia kipato Jumuiya na pale watakapokwama ataendea kuwaongezea .


"Wakati nagombea niliwauliza mnataka nini wakaomba mitaji na mimi nimetoa mitaji ya sh.100,000 kwa kila tawi na nitaendelea kushirikiana nao pale watakapohitaji msaada wangu nitaungana nao wafikie malengo," amesema.


Kadhalika Mwenyekiti huyo amechangia ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule shikizi ya Gongo, matofali 1000 na mifuko 20 ya saruji ujenzi wa zahanati ambapo pia ameahidi kuchangia mifuko 1000 na saruji mifuko 10 ujenzi wa shule ya Sekondari Mlingotini.


Awali akizungumza kwenye kikao hicho katibu wa Malezi wa Jumuiya hiyo kata ya Zinga Magdalena Ngowi amewasisitiza wazazi kuwa na upendo kuwasikiliza watoto wao ili kutatua changamoto wanazokutana nazo.


Ngowi amesema mzazi kuwa karibu na mtoto inasaidia kutatua changamoto za ukatili kabla ya hazijaleta madhara.


Amewataka wanachama wa Jumuiya girl kushirikiana kukijenga chama sambamba na kusisitiza malezi bora ili kuwa na kizazi chenye maadili mazuri


Mwisho

No comments: